Kuna wanawake wengi ambao wanaumia katika ndoa zao kwakua tu hawajui kunyamaza, hawajui kuongea kitu mara moja wakanyamaza. Wanapokosewa na waume zao wengi huishia kulalamika zaidi ya kuongea, unapolalamika unakua kama unaomba msamaha na mwisho wa siku ukizidisha kualalamika hata kama mume wako ndiyo kakukosea lakini unabadilika na kuonekana kama vile una kisirani.
Tuchukulie mfano mmoja ambalo ni tatizo la kila siku, mume wako umemfumania, labda hujamkuta na mwanamke moja kwa moja lakini umekuta meseji za ajabu ajabu katika simu yake. Hapo moja kwa moja aunajua kuwa anachepuka, unaamua kumuuliza anakupa sababu, anakuambia uongo mzuri tu ambao kwa namna flani ni kama vile unamuamini. Sasa huna mpango wa kumaucha mume wako, lakini hunyamazi.
Kwamba umemfumania kweli, labda kaomba msamaha au kakudanganya na wengine wananyamaza kimya. Kwa wanwake wengi suluhu ya karibu ni kulalalamika na kuendelea kumfuatilia katika simu. Hilo ndiyo kosa la kwanza, unapolalamika halafu huondoki unaanza kuwa kero wewe. Kwamba yeye kakukosea kuchepuka hilo ni kosa la zamani, wewe unamkosea kwa kumnyima amani kulalamika kila siku, hilo ni kosa jipya tena la kila siku.
Hapa unajua ni nini kinatokea, mume anakuzoea, anajua wewe ni mtu wa kulalamika, anajua mke wangu anakisirani hivyo haoni makosa yake. Hii ndiyo maana wanaume wengi huona kama ni kawaida kuchepuka na husingizia ni kwakua wake zao wana visirani. Unahaki ya kukasirika, una haki ya kuongea, lakini ongea mara moja, kasirika mara moja hapo mwanaume lazima aweze mara mbili.
Post a Comment