KAMA MMEYAANZA HAYA KABLA HATA YA KUOANA BASI ACHANA NA HAYO MAHUSIANO, COZ MKIOANA NDOA AITAWATESA - EDUSPORTSTZ

Latest

KAMA MMEYAANZA HAYA KABLA HATA YA KUOANA BASI ACHANA NA HAYO MAHUSIANO, COZ MKIOANA NDOA AITAWATESA

Kama upo kwenye mahusiano ya kawaida tu na mwanaume amekutambulisha kwa ndugu zake ila bado ndoa, kama unaona kuwa mahusiano yenu yana matatizo kiasi kwamba hata kabla ya ndoa mshaanza kuwashirikisha ndugu kuwaamulia. Yaani magombana kiasi kwamba unafikia ghatua unamuambia Mama yake, baba yake au ndugu zake mnakalishwa vikao kusuluhishwa, kama si vikao vya kulazimishwa kuhudumia mtoto (kama mliza kabla ya ndoa) basi kimbia.
Narudia ukiona mshaanza kuita ndugu hata kabla ya ndoa basi huyo si mwanaume ni kichomi, kimbia hamtawezana! Lakini kama utaenda kwa ndugu halafu wakaishia kukuambia Vumilia huyo ndiyo alivyo, ndugu wamume wanakuambia umvumilie ndugu yao kabla hajakuoa. Lakin hawaishi hapo wanamalizia mkioana atabadilika, hapa dada yangu sio tu ukimbie, tafuta nauli panda basi ondoka tena kama unaona litakuchelewesha basiruka kabisa!


BONYEZA HAPA KUPAKUA APP YA UTAMU KITANDANI UJIFUNZE MENGI KUHUSU MAPENZI 
Ukiona ndugu wa mume wanakuambia vumilia atabadilika basi jua kuwa hao ndugui washajua kuwa ndugu yao ni kimeo na wanaamini kuwa wewe ndiyo mwanamke Kiazi pekee ambaye utamvumilia. Wao wenyewe washamchoka na washakuchona na wewe hiyo shitaki shitaki yako. Wakiwa wenyewe wanakusema na kusema hutu mwanamke naye mpumbavu atamvumiliaje ndugu yetu huyu? Lakini wakiwa na huyo mwanaume huwa wanamuambia “Huyu naye akikuacha hutapata mwanamke mwingine mjinga wa kukuvumilia wewe mchezee tu!”
Kudhani ndugu wa mume wanakuambia hivyo kwakua wanakupenda, ni sawa na kudhani labda watu wanajenga vyoo kwakua wanapenda vinyesi, hapana nikwakua wanatafuta sehemu ya kusitri takataka zao, wanajua wakiacha vizagae itakua shida. Hivyo hivyo ndugu wa mume, hawakuambii vumilia kwakua wanakupenda bali wanakuambia vumilia kwakua wewe ndiyo utamsitiri ndugu yao, wewe ndiyo choo cha ndugu yao, wanajua ukimuacha ataharibikiwa itakua ngumu kwake kupata mtu mwingine wakuvumilia upuuzi wake!


BONYEZA HAPA KUPAKUA APP YA UTAMU KITANDANI UJIFUNZE MENGI KUHUSU MAPENZI 

Image may contain: one or more people




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz