JITAHIDI UWE MKWELI KWA MPENZI WAKO KUHUSU MAISHA YAKO HALISI ACHA KUMDANGANYA.

Kuwa mkweli kwa mwenza wako kuhusu maisha yako, acha kumdanganya kwamba familia yenu ina uwezo mkubwa wakati ni ya kawaida, kuwa mkweli, mapenzi si utajiri, ni hazina iliyojificha ndani ya moyo.
Kama anakupenda, atakupenda tu, ila siku akigundua kwamba unamdanganya, pendo lake litapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Jieleze kwa uwazi na ukweli kutoka ndani ya moyo wako, naye atakuheshimu na utakuwa umetengeneza mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye ndoa isiyo na migogoro.
Share


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post