Jinsi ya kumpagawisha mpenzi wako, kumteka moyo na akajikuta anakupenda Zaidi na Zaidi.

Mapenzi ni Zaidi ya hisia, Zaidi ya kile mpenzi wako anachokiona na kuhisi akuangaliapo, ni jinsi alivyoridhika kwa kila kitu nakukuona wewe upo Zaidi ya jinsi ulivyo, kiasi cha hisia zake kuzidi na kuwaZaidi ya yeye kuweza kuelezea, kiasi kila akuangaliapo anashindwa kujizuia Zaidi ya kutabasamu.


Na kila ukiwa haupo machoni kwake kwa hisiaunazomsababishia anajikuta anakuwaza na kukufikilia wewe sababu ya kile kilichomoyoni mwake ni Zaidi ya mapenzi, ni Zaidi ya upendo, ni Zaidi ya historia yakuwa pamoja, ila ni uhuru wa kukupenda wewe kwa jinsi atakavyo, uhuru wakuongea na wewe kwa kila hisia ya neno na matamshi, ni utashi wa kupenda nakuyafurahia mapenzi na kuyafanya awe na raha kuyaacha yamtawale moyo nakukufanya wewe umtawale moyo wake kwa kila pigo linalompiga.

Kiumeni.com tunachokuambia sio sura yako au swaga zako ndo zitakazo mfanya msichana akupende Zaidi ya yeye atakavyo, ila ni kwa jinsi wewe unavyomfanya ajisikie akiwa nawe, jinsi anavyojihisi na kupokea upendo unaotoka moyoni kwake na kuukubali, ndicho kitu kikuu kitakacho mfanya mpenzi wako apagawe nawe na kujikuta akikupenda kupitiliza.

Yafanye mapenzi kwa mpenzi wako yawe zaidi ya hisia, zaidi yajinsi anavyojisikia akiwa na wewe, mfanye asipokuona aanze kukufikilia sio kwajinsi anavyokukosa pekee ila kwa jinsi anavyokosa zile hisia za furaha naupendo, hisia za uhuru wa kupenda, upendo uliomtamu maana unamfanya afurahiemapenzi, afurahie maisha kwa ujumla anayotumia na wewe, jinsi mnavyoongea,jinsi ulivyojenga ukaribu na yeye kiasi tofauti na mapenzi yalivyo, mna urafikitayari ulioshiba na kuelewana.

Hakikisha kila mda unaotumia nae unamtengenezea kumbukumbu nzuri, afurahie vitendo mnavyofanya pamoja na kutengeneza historia yenu wawili, kumbukumbu zinazomburudisha moyo wake kiasi hata ukiwa mbali na akazifikilia, zinamfanya atabasamu na hisia za kukumisi kumjaa mara dufu, hizo hisia za kumtaka awe tena karibu yako zimfanye asiache kukutafuta kwenye simu na kukutumia meseji.


Mfanye ajione tofauti, ajihisi unamwona spesho na sio kwa sifa unazompa ila kwa jinsi unavyomchukulia, aone kwa vitendo, aamini kwa macho yake mwenyewe, hii itamfanya akupende bila kujihisi, afanye vitu kwa jinsi mapenzi yanavyompeleka yeyewe, ajitoe kwa moyo na kukuona kuwa nawe ni bahati hivyo atajikuta anaitumia hio bahati kwa marefu na mapana, huku akiwa ajiulizi wala kujishuku.

“mara nyingi wanawake huwa na hofu ya kupenda, hofu ambayoinawatawala Sana na iwapo huwa unawasikiliza kwa makini utakuwa umeshaisikiahofu hii, sababu kuu ya hofu hii ni kuwa, wanawake wanaogopa kutendwa, wanahisiwakimpenda mwanaume kupitiliza, na huyo mwanaume akajua kutamfanya huyomwanamme kumshusha thamani mwanamke”,


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post