Kama wengi wetu tujuavyo, Ndoa ya kwanza ilifungishwa pale Edeni na Mungu mwenyewe. Na ilikuwa ndoa takatifu, iliyobeba msingi na dira ya ndoa nyingine zote zitakazofuata jinsi zinavyopaswa ziwe.
Katika ndoa ile ilihusisha Mtu mume mmoja (Adamu) na mtu mke mmoja (Hawa)..Kwa kupitia wazazi wetu hawa wawili ndio sisi sote tumetokea…ikiwa na maana kuwa ndoa kamili na takatifu inahusisha mume mmoja na mke mmoja…na si Zaidi. Hicho ni kigezo cha kwanza na cha muhimu.
Pia kabla ya ndoa ile kufungishwa, Maisha yalianza na Adamu kwanza, Mungu alimpa Adamu mimea, mashamba ya kulima, makazi na kila kitu, hapo kabla Hawa hajatokea…na Adamu akaanza majukumu yake ya shughuli pale Edeni kabla ya Hawa kutokea…Na Hawa alipotokea alikuwa kama msaidizi tu wa kazi ambayo tayari ilikuwa imeshaanza. Ikiwa na maana kuwa Mwanamume yoyote kabla hajadhamiria kuoa ni lazima angalau awe na mahali pa kujishikiza ili aweze kumhudumia huyo mkewe anayekuja kumwoa…
Na kumbuka Mungu hakumleta Hawa kwaajili ya tamaa za mwili za Adamu, hapana bali alimleta ili awe msaidizi kwake, kwa namna zote, kifikra, na hata katika kazi zake za kimaendeleo Adamu alizokuwa anazifanya…Ikiwa na maana kuwa lengo la kwanza la ndoa sio kukutana kimwili kama inavyochukuliwa sasa na wachache wasio na maarifa ya kutosha.
Hivyo mwanamke jukumu lake kubwa katika ndoa ni kushirikiana na mume wake, na kuyafanya majukumu yote ambayo mume wake angepaswa ayafanye, ikiwemo ya kihuduma na ya kiuchumi, Hawa hakupelekwa kwa Adamu kumtoa Adamu pesa!..bali awe msaidizi….Maana yake kitu ambacho hakijakaa sawa au hakijakamilika mikononi mwa mwanaume, mwanamke anakiweka sawa na kukimalizia.
Na jukumu kubwa Zaidi mwanamume na mwanamke walilopewa ni kujiepusha na Uovu…Na shetani huwa anawatumia wanawake wengi kuharibu ndoa kuliko wanaume..Kama Hawa mzazi wetu wa kwanza angekaa katika nafasi yake na kujiepusha na uovu, leo hii duniani kungekuwa ni paradiso, lakini kwa kuacha majukumu yake ya USAIDIZI na kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu hakumwagiza matokeo yake ndio yakawa yale…Na hata sasa mwanamke akiacha majukumu yake na kujikita katika ulimwengu huu, katika usengenyaji, umbea, katika kutoa siri za mume wake nje, katika kutomheshimu mume wake, kumdharau, kumdhalilisha, kumwaibisha, kuvaa kikahaba, kuwa mhuni, mlevi,mtu mwenye mizaha na kila aina ya udunia, anajiharibia mwenyewe na anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..
Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.
Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…
Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…
Hata Hawa alipotolewa ubavuni mwa Adamu, Bwana Mungu aliparudishia nyama pale palipotolewa ili Maisha ya Adamu yaweze kuendelea, hakuacha shimo pale wala kidonda!…Na hali kadhalika unapomtoa mwanamke kwa wazazi wake ni lazima uzibe pengo uliloliacha pale, na hilo unaliziba angalau kwa mahari, sio unamwiba na kuacha huzuni kule na malalamiko na laana na maumivu.
kama utashindwa kulipa mahari ya kiasi hicho kidogo cha fedha utawezaje kuitunza na kuihudumia familia yako inayokuja huko mbele, ambayo pengine itahitaji matunzo ya gharama nyingi kuliko hizo za mahari??…kama hutaki kutoa mahari, maana yake bado hujaelewa maana ya kuoa, hivyo unapaswa ungoje mpaka utakapoelewa vyema maana ya ndoa ndipo uoe.
Na mwisho biblia inatuambia kuwa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana…wale ambao wameoa na wawe kama hawajaoa…ili muda mwingi tuutumie katika kuutafuta Zaidi ufalme wake na haki yake kwasababu unyakuo upo karibuni, na mbinguni tuendako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, yatakuwa ni mambo mapya huko ambayo ni ya muhimu Zaidi kuliko haya.
1Wakorintho 7:28 “Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
29 Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.
31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha n a mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”
29 Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.
31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha n a mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”
KAMA UMEOLEWA NA HUJUI NI WAKATI GANI WA KUNYAMAZA BASI UNAIVUNJA NDOA YANO!
Kuna wanawake wengi ambao wanaumia katika ndoa zao kwakua tu hawajui kunyamaza, hawajui kuongea kitu mara moja wakanyamaza. Wanapokosewa na waume zao wengi huishia kulalamika zaidi ya kuongea, unapolalamika unakua kama unaomba msamaha na mwisho wa siku ukizidisha kualalamika hata kama mume wako ndiyo kakukosea lakini unabadilika na kuonekana kama vile una kisirani.
Tuchukulie mfano mmoja ambalo ni tatizo la kila siku, mume wako umemfumania, labda hujamkuta na mwanamke moja kwa moja lakini umekuta meseji za ajabu ajabu katika simu yake. Hapo moja kwa moja aunajua kuwa anachepuka, unaamua kumuuliza anakupa sababu, anakuambia uongo mzuri tu ambao kwa namna flani ni kama vile unamuamini. Sasa huna mpango wa kumaucha mume wako, lakini hunyamazi.
Kwamba umemfumania kweli, labda kaomba msamaha au kakudanganya na wengine wananyamaza kimya. Kwa wanwake wengi suluhu ya karibu ni kulalalamika na kuendelea kumfuatilia katika simu. Hilo ndiyo kosa la kwanza, unapolalamika halafu huondoki unaanza kuwa kero wewe. Kwamba yeye kakukosea kuchepuka hilo ni kosa la zamani, wewe unamkosea kwa kumnyima amani kulalamika kila siku, hilo ni kosa jipya tena la kila siku.
Hapa unajua ni nini kinatokea, mume anakuzoea, anajua wewe ni mtu wa kulalamika, anajua mke wangu anakisirani hivyo haoni makosa yake. Hii ndiyo maana wanaume wengi huona kama ni kawaida kuchepuka na husingizia ni kwakua wake zao wana visirani. Unahaki ya kukasirika, una haki ya kuongea, lakini ongea mara moja, kasirika mara moja hapo mwanaume lazima aweze mara mbili.
Post a Comment