Moja ya dalili kubwa ya mtu uliyenae kuwa anakupenda, ni heshima anayokupa. Heshima ni nguzo ya upendo katika mapenzi yoyote yale, maana huzalisha neno linaloitwa kipaumbele.
Wapenzi wanaoheshimiana, daima hakuna neno ubinafsi bali jambo lao ni lao na si la mtu mmoja mmoja. Maana kila mmoja ulipa kipaumbele jambo la mwenzake.
Upendo huonyeshwa kwa vitendo, na moja ya matendo makubwa ya upendo ni ile heshima unayoipata kutoka kwa mpenzi wako, na ile unayoitoa wewe.
Mpenzi wako anapokuambia ninakuheshimu, ni vinzuri akaonyesha kwa vitendo. Na hiyo ndiyo dalili ya kuwa, mpenzi wako anakupenda kweli na si kwa maneno tu.
Siku zote heshima inapoanza kupungua katika upendo wenu, ni moja ya dalili kubwa ya kuanza kuchokana.
Kumbuka yeyote anayekupenda, basi atakuheshimu. Na mwenye kukuheshimu kila wakati, huyo ndiyo mwenye mapenzi ya dhati kwako. Maana atakujali na kukuthamini kwa jinsi ulivyo.
Post a Comment