Jambo moja kubwa kwa mtu umpendae au akupendae ...
Ni mtu wa kwanza yeye au wewe kumfikiria katika akili yako asubuhi unapoamka.
Usishangae wewe au yeye kukuuliza unaenda wapi, nini unafanya, uko na nani ...hayo ni maswali ya kawaida sana kwa mtu anaekupenda ..na muda mwingine hata kama yanakukera inabidi uyazoee....maana anajali.
Haijalishi atakuwa na ubize gani katika kazi zake ...lazima atatafuta muda wa kukujulia hali ...maana anahisi moyo wake hauko salama kama ajakutafuta na kujua unaendeleaje na siku yako...na huu ndio moyo haupendi kujificha kwa mtu unaemjali.
Atatafuta namna yoyote ya kuwa mwaminifu kwako kwa mambo yanayowahusu nyie wawili ..hii ni kwa sababu hataki kuona yeye kuwa chanzo cha kuharibu upendo ambao upo kati yenu... Kwa namna moja ama nyingine atataka kubeba majukumu ya kulinda hisia za upendo wako kwake.
Dayari Yangu
Dayari Yangu
Post a Comment