JAMBO KUBWA WANALOKOSEA WANAWAKE WANAPOINGIA KWENYE MAHUSIANO.

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini wanapotambua kwamba wameshaoa hushangaa sana na huumia na kusema wanaume wote ni mbwa tu. Wanaume sio mbwa ni sisi wenyewe ndio tumeshindwa kufanya uchunguzi. Tulishaambiwa kwenye kila mafanikio ya Mwanaume nyuma yake Kuna mwanamke!!! Na wewe unataka Mwanaume mwenye mafanikio unategemea nini??? Huyo sio mumeo mtarajiwa huyo ni mume wa mtu Fulani Ni agharabu sana kukutana na Mwanaume anayejiweza akawa single, either uwe shareholder au unyanganye share ya mwanamke mwenzio kitu ambacho sio busara. Mume wako yupo anahangaika kutoka kimaisha anapigania ndoto zake. Huenda yuko shule, shamba, dukani au anabeti kimsingi yupo anapigania kuchomoka Kimaisha. Anakusubiri tu wewe umpe support na back up ya kutosha mtafute huyo uanze nae chini.
Shea kwenye magroup kuwakumbusha mabinti


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post