Ishara za uhakika za mchumba mwenye mapenzi ya kweli na wewe na anayekupenda kweli:


Je mchumba wako anakupenda kweli?
Zifuatazo ni ishara za mchumba wa kweli
1. Anakuheshimu na anakufanyia mambo yote kwa heshima.
2. Muda wote uko kichwani kwake/anakuwaza wewe.
3. Anakusikiliza na kufanya unachokisema baada ya kupima na kutoona kasoro na akiona atakushauri kwa staha.
4. Anaweza kukushika mkiwa mnatembea bila kuogopa watu. mfano, mkono mkiwa sehemu zenye watu wengi.
5. Anakujali kwa chochote kiwe kingi ama kidogo.
6. Anataka uipende na ushirikiane na familia na ndugu zake.
7. Anaweza kuomba msamaha bila shuruti pindi anapokukosea.
8. Akiwa anaongea badala ya kusema nita…. anasema tuta…. mfano, tutafanya hivi badala ya nitafanya hivi.
Huyo sio mbinafsi oana nae haraka.
9. Anakuweka kwenye mipango yake ya baadae akitambua wewe ni sehemu ya maisha yake.
10. Anasema ‘SASA’. (Mfano SASA tufanyeje?) Anatumia neno sasa kukupa nafasi ya kutoa mawazo yako.
Wewe una mwenza wa aina gani?


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post