Hizi Ndio Sababu Zinazowafanya Wanaume Kufa Mapema Kabla ya Wanawake. - EDUSPORTSTZ

Latest

Hizi Ndio Sababu Zinazowafanya Wanaume Kufa Mapema Kabla ya Wanawake.



Zifuatazo ni sababu 5 za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.

1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.


2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

3. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao
waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

4. Ugumu katika kujali afya.

Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.
Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.

5. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa
moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.

Kuwa open, roho safi and less agressive.


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz