Yawezekana kila kukicha mwili unakuwa mzito hadi unashindwa kuamka sababu ya maumivu ya moyo kuhusu sintofahamu inayoendelea kwenye mahusiano yako.
Mchana unashinda bila furaha yoyote na kila unachojaribu kufanya unaona hakiendi sababu migogoro imekuwa ni sehemu ya maisha yako na hujui jinsi gani ya kuitatua.
Giza linapoingia basi mambo huzidi kuwa mabaya na hata unapojaribu kulala usingizi hauji sababu kichwani msongo wa mawazo umejaa na huna majibu ya maswali unayojiuliza.
Mahusiano yamekukosesha maana ya maisha, mbele huoni mwanga bali ni giza tuu! Kila unapojaribu kupiga hatua unaona hamna pa kuelekea na unazidi tuu kubaki njia panda.
Mpendwa! Utaishi kwenye mahusiano yasiyo na mwelekeo hadi lini? Utaendelea kuishi na maumivu ya moyo bila kuitua mizigo hadi lini? Huoni kama unajikosesha haki yako ya kufurahia mahusiano?
Nikwambie tuu mpendwa amua sasa uwe ni wakati wa kupata tiba, ushauri na mwongozo wa kisaikolojia ili maisha yako yawe yenye maana. Wakati ni wako sasa! Amua kuishi maisha ya tofauti na ufurahie mahusiano yako.
Post a Comment