HII NI KWA WADADA AMBAO MNATAFUTA NDOA; NAMNA YA KUKWEPA KUUMIA SANA KATIKA MAHUSIANO

Photos From Banky W and Adesua Etomi's Wedding Introduction ...
Sijui wewe lakini hivi ndivyo nilivyoona mimi na katika kazi zangu mimi hiki ndiyo kinachokutana. Mwanaume anapowaza kuhusu ndoa moja kwa moja akili yake huwaza kuhusu kujitegemea.
Atawaza kuhusu kuwa na kazi nzuri yenye kipato cha kumuwezesha kuhuduia familia yake tarajiwa, atawaza kuhusu kuwa na nyumba au hata chumba cha kupanga, atawaza kuhusu kila kitu namna ya kuhudumia mke.
Lakini mwanamke anapowaza kuhusu ndoa, anawaza mwanaume ambaye atimizia mahitaji yake yote, ambaye atakua na nyumba au chumba, ambaye ana kazi ya kumuingizia kipato na mambo mengine kama hayo.
Nijambo la kawaida sana kukuta mwanamke sanaolewa akiwa hana kazi ya kumuingizia kipato, au hata kulazimika kuacha kazi ili aolewe lakini ni nadra sana kukuta mwanaume anaoa akiwa hana kazi.
Ninadra zaidi kukuta mwanaume anaacha kazi ili aoe, ngumu sana na hata kumpata huyo mwanamke ambaye atavumilia mwanaume mabaye hana kazi itabidi ufanye kazi ya ziada.
NINI KINATOKEA HAPA?
Kinachotokea hapa nikua mwanaume anapotaka kuoa huwekeza katika maisha yake binafsi, anakua na kila kitu chake hivyo hata kama akiachana na mwanamke anachopoteza tu ni mwanamke na si kingine.
Kwamba mwanaume anapoishi na mwanamke kama mpenzi tuseme miaka mitatu, katika miaka mitatu hiyo atakua amewekeza vitu vingi kiuchumi hivyo hata akiachika anampoteza mwanamke tu na maisha yake hayabadiliki.
Sana sana atatafuta mwanamke mwingine tu basi. Lakini mwanamke anapokua kwenye mapezi basi hawekezi kuhisia tu bali kimalengo, yaani badala aya kujiwekea malengo ya kufanikiwa mwenyewe huweka malengo ya kufanikiwa na yule mwanaume.
Hivyo kwake mwanaume akifanikiw ana yeye hujiona kama amefanikiwa na hata kusahau kua wanaweza kuachana na wakiachana haondoki na kitu kwani huyo mwanaume si mumewe.
Hii ndiyo maana mwanamke akiachwa baada ya mahusiano ya kama miaka mitatu tu, anajikuta anaumia zaidi kwani kapotezewa muda mwingi na kashindwa kufanya mambo binafsi.
UFANYE NINI SASA?
Kwamba kama uko kwenye mahusiano, mwanaume haeleweki labda anakupenda lakini haongelei ndoa, unajaribu kumshawaishi lakini anasema kua hajajipanga na vitu kama hivyo.
Hajasema hakuoi, hajasema hakutaki wala nini? Hakuonyeshi dalili kua hakutaki au haonyeshi kua na mtu mwingine. Nasema hivyo kwakua kama umeona dalili kua ana mtu mwingine.
Kama ameshakuambia hawezi kukuoa, au kashasema yeye si muoaji basi wewe ni kuondoka tu, labda kama na wewe unamchezea tu lakini kama uko siriasi basi ondoka.
Usikae na kusubiri ndoa, usisimamishe mambo yako na kusubiri ndoa. Anza maisha yako, hembu anza kutafuta kazi ya kufanya kama huna, tafuta kitu cha kukuingizia kipato.
Hilo ni la kwanza lakini la pili anza kuwekeza katika maisha yako, usikae na kusubiri kua labda atakuoa, labda ana kitu flani kwahiyo mimi sihitaji kuwa na kitu hicho hapana.
Kama unafanya kazi au biashara wekeza muda wako mwingi katika kujiimarisha wewe kiuchumi. Hili ni la muhimu sana, kujiimarisha kiuchumi.
Unaweza usione umuhimu wako sasa lakini itakupa furaha zaidi kama ukiw ana vitu vyako, kama ukiweze ku8jitegemea na ukiwa na maamuzi yako.
Mwanaume hatakusumbua na wala hatakuumiza kichwa kwani utakua umeielekeza akili yako sehemu nyingine zaidi ya kumsubiria yeye aamue kukuoa na ndiyo maisha yako kuanza.
LABDA NIKUAMBIE KITU?
Unachanganyikiwa zaidi kuhsu ndoa, kuhusu msimamo wake kwakua maisha yako hayajaanza. Kunavitu umevisimamisha kwasababau unaamini unatakiwa kuvifanya baad aya ndoa.
Labda nikupe mfano, inawezekana bado unaishi nyumbani kwenu, unamtegemea Baba yako, hivyo umechoka na ile hali ya pale nyumbani, huna uhuru wa kufanya mambo yako, unataka kuwa na familia yako.
Hivyo unaona njia rahisi ni kuolewa sasa kama hakuoi unaona kama unachanganyikiwa. Lakini inawezekana umepangisha chumba lakini huyo mpenzi wako ndiyo anakuhudumia kwa kila kitu.
Ndiyo hapo anakupa kila kitu lakini hakuoi, unachoka, kwani pesa zako zinaishia saluni tu na kwenye vitu ambavyo si vya msingi. Lakini unataka kuolewa kwakua hutaki kuhudumia bali kumiliki.
Hapa namaanisha nini, una mpenzi kakupangia nyumba, wewe si mkewe, labd amna mtoto anawahudumia, lakini wewe si mkewe, hii inamaanisha kuw ahuna uhuru na kila kitu chake.
Sasa anakupa vitu anavyotaka lakini akikuoa vinakua vyako, vinakua venu. Hiki ndiyo kitu kinachokuchanganya, lakini ungeelekeza akili yako katika kutafuta vyako, ukaielekeza katika maendeleo yako anakuhudumia lakini humtegemei.
Akili ingepanuka na wala usingepata ile presha ya kutaka kuolelewa, ungekua unawaza maisha yako, kupata vyako, kuwekeza zaidi hivyo usingeboreka kukosa vitu vyake.
LAKINI ANAWEZA KUKUACHA!
Najua hili hutaki kuamini ila hakuna garantii katika mapenzi, inawezekana anakupenda sana sasa lakini haimaanishi ni lazima akuoe, kuna wengi tu walikua wanapendwa kuliko wewe na waliachwa.
Hapa sitaki kukukatsiha tamaa kua na wewe utaachwa hapana nakuambia ukweli kua ni kitu ambacho kinaweza kutokea. Sasa hembu mchukulie mpenzi wako kama pochi ya hela.
Ukipoteza pochi yenye shilingi mia tano hutaumiza kichwa sana kama ukipoteza pochi yenye shilingi milioni moja. Unaweza kuchanganyikiwa.
Hapa namaanisha kua utaumia zaidi kama utawekeza nguvu zako, hisia zako, pesa zako na kila kitu kw amwanaume halafu akakuacha. Lakini kama utampenda na kumheshimu lakini pesa zako ukawekeza kwako hutaumia sana.
Utaumia kumpoteza yeye lakini si kuumia kupoteza mali zako, kwamba nikama kwenye pochi utaumia kupoteza pochi lakini kama haikua na hela nyingi hutaumia kupoteza pesa.
NADHANI UMENIELEWA!
Sijui lakini nadhani umenielewa, badala ya kukaa kuwaza kuwa atanioa lini hembu badilika na waza kuwa nitafanya nini ili kubadiliisha maisha yangu
Fanya mambo ya maendeleo,wekeza katika maendeleo yako kwanza na kama ni kukuoa atakuoa muda ukifika, hakuna namna utakavyomlazimisha mwanaume kukuoa hata kama ni kwa kubeba mimba.
Endelee kutafuta, usiweke rehani ndoto zako, usipuuzie ndoto zako na kuziacha zife kisa mwanaume. Hapana timiza ndoto zako na atakukuta njiani.
MUULIZE MIPANGO YAKE!
Ndiyo kuna wkaati inabidi uulize, umekaa na mwanaume miaka mitatu haeleweki halafu bado unasubiri aoteshwe ilia je kukuoa hapana. Muulize anasuburi nini, ana mipango gani.
Lakini sio tu kama anamipango gani hapana muulize kama wew eupo katika mipango yake. Hapa simaanishi umuambie akuoe, au akuambie kama atakuoa au la hapana.
Hapa unamuuliza kama anamipango na wewe au uweke mipango yako mwenyewe. Acha kuishi kwa matumaini kua labda siku atakuoa atakufanya uwe sehemu ya maisha yake, uliza na ujue nini cha kufanya.
Kuwa tayari kupokea jibu lolote na kama unamipango yako ya maendeleo, umewekeza kwenye mambo yako hutaumia sana na ni rahisi kuendelea na maisha yako, uataumia kweli lakini utawahi kupona.
Imeandikwa Na. Brayton official love


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post