Habari za wakati huu wadau,nayazungumza haya kwa uzoefu. Inasemekana kwamba asilimia kubwa ya wanaondoa hawa-enjoy maisha yao ya ndoa kwa sababu kadha wa kadha, wengine wakidai kuwa ndoa nyingi za karne hii zimetawaliwa na usaliti hasa kwa wanaume, kwa lugha ya mtaani wanaita "michepuko" na kadhalika na kadhalika. Huenda kuna ukweli ndani yake, lakini hebu tutazame nini hasa kinaweza kusababisha hiyo michepuko.Kumbuka unapooa/kuolewa, wewe unakua sio mwanamke wa kwanza kwa huyo anayekuoa au sio mwanaume wa kwanza kwa huyo unayemuoa, wote hao walishakua na mahusiano ya awali. Na mbaya zaidi huenda hao waliokua nao awali walitamani ndoa wakakataliwa, hapa namaanisha mwanamke wa awali wa huyo ambaye kwa sasa ni mumeo alitamani sana ndoa na huyo mumeo lakini ukabahatika wewe au mwanaume wa awali wa huyo ambaye sasa ni mkeo alitamani ndoa na huyo mkeo lkn ukachaguliwa wewe. Katika mazingira kama haya, ile siku ya harusi yako especially kwenye ile segment ya kuwashika mkono maharusi na kutoa zawadi.Usikubali huyu mwanamke ambaye hakubahatika ndoa na mumeo au huyu mwanaume ambaye hakubahatika ndoa na mkeo akukumbatie anapokuja kukushika mkono wakati wa tafrija ya ndoa yako, kwasababu inasemekana anapokukumbatia hukuachia madawa ya kuharibu ndoa yako wengi wao ni washirikina. Lakini pia inawezekana ukawa hujui kwamba fulani ndio alikua mpenzi wa zamani wa huyo mumeo au wa huyo mkeo, njia salama hapa ni kuwashika mkono tu wageni waalikwa wote na kuwakumbatia wale ambao ni ndogo zako wa karibu ingawa pia sio wa kuwaamini sana kwasababu huwezi kujua nani anakuombea maisha mema ya ndoa. Wanasema "kumbato/kumbatio" ndio njia nyepesi sana ya kulogea, so kama ameenda kwa mganga akikukumbatia tu dawa inakamata saa hiyohiyo. Zawadi: Hakikisha zile zawadi zote utakazopata siku ya harusi yako zinaobewa kabla hujaanza kuzitumia cause nyingine zina malimbwata. So usije ukamuona mumeo/mkeo anachepuka sana ukaanza kusema Mungu hajakupa mume/mke bora, wakati mwingine ni nguvu za kibinadamu (kishirikina) zinaharibu ndoa yako.Nimeshatimiza wajibu wangu, usije sema hukuambiwa.

Post a Comment