Hakuna mwanaume aliye single ambaye kila siku akitoka nyumbani kwake anajisemea ngoja nitafute mke kama vile anavyotafuta funguo, simu au fedha aliyopoteza. Haipo hiyo.
Mwanaume siku zote anataka awe na mwanamke katika uchumba na katika safari hiyo ya mahusiano wazo la kukuoa wewe au mwingine humjia kutokana na namna alivyo-expirience mahusiano hayo.
Na pale mwanaume anapokuchagua wewe, huwa ni wewe tu anayekuhitaji. Wala mwanamke hutatumia nguvu nyingi kuyafanya mahusiano hayo yanyooke. Sasa baadhi ya wanawake wamejipa hadi kazi ya ushushushu wa kutafuta ni nani anatoka na mwanaume wake, na wanapobaini unakuta wanamchimba hadi mkwara huyo wanaembaini. Hiyo haisaidii kama mwanaume mwenyewe hana jitihada ya kusimamia mahusiano hayo.
Ndio maana mahusiano mengi yaliyosimama ni yale ambayo Mwanaume ameamua kuyasimamia kidete kuhakikisha mwanamke wake anayo furaha.
Wanawake wengi labda kwa kunogewa na mahusiano wamekuwa wakijiachia mno, kuwa-post wenza wao kwenye mitandao ya kijamii na wengine kufikia hatua ya kuwazalia kabisa wakiamini kuwa hao ndio tayari wanaume zao wa ndoa. Lakini baadae kinachokujaga kuwatokea anajua Mungu mwenyewe.
Dada zetu wajifunze kuwa na uvumilivu, unapokuwa na mwanaume kwenye mahusiano usijione kama ndio umeshafika, ukahamisha na akili zako zote bila kufikiria mustakabali wa maisha yako. Jifunze kuwa na kifua cha kuficha mambo mpaka pale utakapoona kuna uelekeo chanya wa mahusiano hayo.
Unavyoingia katika Mahusiano, beba na akili zako, usiziache nyuma. Ni rahisi mno kufahamu u-serious wa mtu katika mahusiano endapo utashirikisha akili yako.
Post a Comment