DEAR LADIES! NISIKILIZENI KWA MAKINI

Ladies:
Tumia muda ulio nao katika maisha yako ku..invest katika kujitambua ..kuliko kutaka kuwatambua watu wengine ambao hawahusiani kabisa na maisha yako...
Kujitambua kwako kutakusaidia kutambua yupi mwanaume anaekupenda na yupi anataka kupoteza muda na wewe. Kujitambua kutakusaidia kujua yupi mwanaume ambae ameamua ku..invest upendo wake kwako na yupi ameamua kucheza na akili zako. Kujitambua kwako kutakusaidia kujua mwanaume anakuchukulia vipi je anakuchukulia kama chombo cha starehe au anakuchukulia kama mwanamke anaemueshimu. Kujitambua kwako kutakusaidia kujua kuwa mwanaume huyu mimi ni zawadi kwake au mimi ndie naemuitaji sana kuliko yeye anavyonihiitaji, kujitambua kwako kutakusaidia wewe kujiamini katikati ya genge la wanaume walaghai ....then ukishajua hayo ni lazima na wewe ujue kuwa wewe ni binadamu unaehitaji nafasi katika moyo wa mtu mstaharabu...mtu ambae wewe utakubali kuwa msaidizi wake katika maisha yako yote ...nae atakubali kuwa wewe ni moja ya zawadi kubwa ambayo haijawahi kutokea katika maisha yake...
Na Mungu atusaidie...
#DayariYangu


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post