Dalili za hatari katika #UCHUMBA


IKIWA uhusiano wako wa #UCHUMBA unakufanya ukasirike na kutokwa na machozi kila wakati, unafaa kuelewa kwamba mambo sio mazuri.
Na ikiwa tabia za mchumba wako zinakukosesha furaha, kukusononesha bure, basi usiwe king’ang’anizi, jitoe; tena haraka🏃
#Tabia zinazokosesha mtu furaha katika uhusiano hubadilika na kuwa maafa.
Ni tabia kama hizi zinazofanya watu kuua wachumba wao. Hivyo basi, watu wanafaa kuwa waangalifu ili kuepuka maafa.
tabia kama vile kupandwa na hasira kwa sababu ya mambo madogo, kukunyima uhuru wako na kukuchukulia kama mali yake binafsi, zinaweza kuzua maafa.
Ukigundua kuwa mchumba wako anahisi kwamba anakumiliki sawa na mali yake nyingine kiasi cha kukunyima uhuru wa kufurahia maisha kama vile muda wa kujumuika na marafiki, kukunyima nafasi ya kujieleza na kukutaka kufuata maagizo yake kila wakati, basi unafaa kutahadhari na kuchukua hatua mapema ili kuepuka hatari inayoweza kutokea baadaye.
WATU kukatiza uhusiano wakigundua wachumba wao wana tabia kama hizi kwa sababu walio nazo huwa vigumu kubadilika.
Usisubiri hadi ujutie. Katiza uhusiano ukigundua kuwa mtu wako ana tabia zinazoweza kuweka maisha yako hatarini. Makosa ya wengi ni kukwama kwenye kitu #Mapenzi hata ikiwa tabia zake ni za kikatili
WANAWAKE na WANAUME, wote wanaweza kuwa na tabia hii. “Wanawake wameua wachumba wao sawa na wanaume kwa sababu ya hasira, tuhuma na kukaidi maagizo yao,.
WATU wanafaa kuepuka Wanaume au Wanawake wanaokosoa kila kitu Wengine wanachofanya au kusema. “Moja ya dalili kwamba mchumba anaweza kuwa hatari ni anapokosa kuona uzuri wowote katika ufanyalo na usemayo. Watu kama hao huwa wanataka kufanya wachumba watumwa wao kwa kila hali.
Wenye tabia hizi huwa wanawashambulia wachumba hao kwa maneno ya kuwadhalilisha.
Ikiwa hakuna unachosema au kutenda kinamfurahisha mchumba wako, basi kuna hatari.
Ugomvi wa mara kwa mara ni dalili nyingine ambayo imekuwa ikizua maafa miongoni mwa wachumba.
Ukigundua mchumba wako anapenda kuzua ugomvi kwa masuala madogo madogo, basi kuwa mwangalifu kwa sababu hana uvumilivu. Watu wenye hulka hii wanaweza kusababisha maafa.
Nashauri kutonyamaza au kuwahadaa watu kuwa uhusiano wenu ni shwari ilhali hali si shwari.
Kuna watu wanaonyamaza au kuficha wanayopitia mikononi mwa wachumha wao wakiogopa fedheha na unyanyapaa hadi pale maafa yanapotokea. Ni muhimu kuzungumza na unaowaamini ili uweze kupata msaada.
Kilele cha tabia hizi ni kwenye ni pale munapoingia kwenye #NDOA , kudharau mwenzake hadi anaanza kumnyima tendo la ndoa. Kulingana hali hii kuacha kufanya mapenzi ni kunyima uhusiano wenu rotuba. Kunyimana tendo la ndoa ni sawa na kunyima uhusiano chakula na maji ya kuukuza. Uhusiano kama huu huwa umekosa rotuba na katika hali hii, hukosa kunawiri na kushuhudia mizozo isiyokwisha.
Ikiwa uhusiano wa mapenzi unakukosesha furaha, kukutenganisha na marafiki na jamaa zako wa karibu, basi kuwa makini na uchukue hatua usije kujuta baadaye majangani.
Uhusiano wa mapenzi unapaswa kuwa wa furaha na sio mateso, dhiki moyoni na majeraha mwilini.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post