DALILI YA KWANZA KUWA MAHUSIANO YAKO YAMEKUFA YANSUBIRI KUZIKWA NI PALE AMBAPO...!

UTAMUZAIDI APP

Dalili ya kwanza kuwa mahusiano yako yameshakufa yanasubiri kuzikwa ni pale ambapo mwanaume anaanza kukuomba pesa, kwamba mwanaume amabye hajawahi kukuhudumia kwa chochote anakuomba pesa na kibaya zaidi nikuwa ukimuambia sina basi ananuna na kukuchunia kwa muda. Lakini dalili kuwa mahusiano yako yameshazikwa zamani watu wapo kwenye matanga ni pale ambapo wewe mwanamke unaanza kumhudumia mpenzi wako kwa kila kitu au kumpa pesa kila anapokuomba na kununa nuna kama ana mimba changa.

Ukiona mwanaume anakuomba omba pesa iwe ni moja kwa moja au kwakulalamika sijui nina shida hii, nina shida ile, sijui hali ngumu na vimaneno maneno ili ujiongeze umpe basi mapenzi yenu yashakufa. Lakini wewe ukijiona unampa jua mapenzi yashazikwa umeshaachwa muda mrefu na vihelahela vyako ndiyo vinamuweka kwako. Wanaume hatuhongwi na wala hatusikii raha kuhongwa. Kama huamini kuwa umeshaachwa, una mwanaume ambaye unamhudumia kama mke wako, hembu acha kumpa pesa wiki mbili tu tena bila sababu muambie sina halafu uone kama hutasikia ana mwanamke mwingine.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post