1. MWANAUME HAPENDI KUFOKEWA: Hata kama amekosea; jaribu kumuonyesha kosa lake pasipo kumfokea au kumvunjia heshima.
2. MWANAUME HAPENDI KUULIZWA MASWALI MENGI KWA WAKATI MMOJA: Ukimuuliza swali halafu yeye anakua kimya au anaduwaa; ujue hana jibu au anajisikia vibaya kuhusu jibu ambalo anatakiwa kutoa. Mpe muda ajipange kutoa jibu.
3. MWANAUME ANAHITAJI MUDA WA KUKAA KIMYA; USIMLAZIMISHE KUONGEA KILA WAKATI: Zaidi sana anapopita kwenye hali ngumu au changamoto fulani; wanaume wengi hupenda kukaa kimya huku akiwaza nini cha kufanya. Tofauti na wanawake, ambao wakati wa changamoto ndipo wanataka kuongea zaidi. Wanaume wengi hawapendi kuongea kama hawana suluhisho la shida iliyopo mbele yao.
4. MWANAUME HAPENDI MKE MWENYE KIHERE-HERE: Yani hata kama bado hajakwambia, kaa ukijua kwamba wanaume hawapendi kuwa na mke ambaye hapitwi na jambo. Mwanamke anayetaka kuchangia kila kitu au kuongea-ongea sanaaaa! Mmmhhh! Unamchosha mwanaume hivyo.
5. MWANAUME HAPENDI MKE WAKE AWE NA MARAFIKI WEEENGIII; ZAIDI SANA MARAFIKI WA KIUME: Wanaume wengi wana WIVU; hivyo mwanaume hapendi kuona mke wake yuko bize “ku-entertain” wanaume wengine (HATA KAMA HAKUNA MAHUSIANO MABAYA). Mara huyu ni rafiki yangu tulisoma nae, niliwahi fanya nae training, ni mwalimu wa kwaya, oohh huyu tulifanya nae kazi, huyu nachati nae tu mtandaoni, bla, bla , bla…!!
6. MWANAUME HAPENDI KUNYANYASIKA: Wanaume wengi ni rahisi kusumbuliwa na hali au hisia ya kujiona duni (Inferiority Complex). Zaidi sana kama MKE ndiye mwenye pato kubwa, au elimu kubwa, umri mkubwa, au anatoka familia yenye nguvu zaidi kuliko ya mume. Hapo inabidi mwanamke awe makini sana maana kitu kidogo tu kinaweza sababisha mwanaume adhanie kwamba tayari anadharaulika. Mwanamke anahitaji HEKIMA ya juu kuishi na mume mwenye shida ya kujidharau.
7. MWANAUME HAPENDI KUPOTEZA MAMLAKA AU SAUTI YAKE KWA MKE WAKE: Yani mke anafanya chochote anachota, anakwenda popote, na hamsikilizi MUME wake. Mwanaume akiona dalili za kupoteza mamlaka yake na kukosa sauti kwa mkewe, basi HUJARIBIWA kutafuta mahali pengine pa kuonyesha mamlaka yake kama mwanaume.
✨NB:
π YAPO MAMBO MENGINE MENGI KATIKA “SAIKOLOJIA YA WANAUME”, LAKINI HAYA NI YA MUHIMU SANA.
‼️- Ni rahisi KUMPENDA Mke mwenye UTII; Vilevile, ni rahisi KUMTII Mume mwenye UPENDO.
✨ MITHALI 14:1; “Kila MWANAMKE aliye na HEKIMA HUJENGA nyumba yake; Bali aliye MPUMBAVU HUIBOMOA kwa mikono yake mwenyewe.”
Post a Comment