Wahenga wanasema raha ya mapenzi umpate akupendae ingawa watu wengi wamekuwa wakiumizwa na mapenzi na watu wanaojulikana kama Matapeli wa mapenzi.
Wapo ambao wamekata tamaa kabisa, hawataki kusikia kitu kinachoitwa ndoa maana kila walipojaribu kutupa karata wamejikuta wakiambulia maumivu. Hivyo wanaona bora kuishi kivyaovyao tu.
Ni vyema kujua dalili za mwanaume ambaye sio muoaji ambaye yupo kwa ajili ya kukuzuga:
1.Atakutafuta Wakati Wa Kukutana kimwili tu
Yupo kwako kwa ajili ya maslahi fulani na baada ya muda atakuacha mtu ambaye yupo kwako halafu hana muda na wewe zaidi ya kukuhitaji tu kwa ajili ya kujiburudisha, huyo anza kumtilia shaka.
2. Mwanaume ambaye sio muoaji atajifanya ni mpenzi wako lakini pia hapendi umjue sana.
Hahitaji uingie kwenye maisha yake kiundani, mnakutana tu barabarani au hotelini biashara imeishia hapo. Hataki kukutambulisha kwa ndugu au hata marafiki. Ukimuona yupo hivyo, anza kuwa naye makini.
3. Hatakuwa na Maongezi ya Maendeleo na wewe.
Wanaume matapeli mara nyingi huwa wanakuwa hawapendi sana kuzungumza mipango endelevu na watu wao. Mwanamke anapoanzisha tu habari hizo, anaruka fasta na kuchomekea mada nyingine. Hayupo tayari, hawezi kukuvumilia uanze kuzungumza habari za sijui kuwa na familia, kuwa na watoto na mambo mengine kama hayo. Anataka mzungumzie zaidi viwanja vya starehe, kula raha na kumaliza mahitaji yake ya kimwili. Baada ya hapo, hana mpango tena na wewe.
4. Atakudanganya kila nafasi atakayopata
Ukimuona mwanaume anakuwa muongomuongo, hana kauli moja katika maisha yenu hiyo pia ni dalili mbaya. Mwanaume ambaye ana nia thabiti ya kuwa na wewe, hawezi kuwa mjanjamjanja. Kama ni sanaa hizo atazifanya kwa watu wengine lakini si kwako.
Post a Comment