Wanawake wa siku hizi hawataki kero, ukimkera tu umeachwa



Habari zenu wakuu,

Nawakumbusha wanaume kwamba wasiishi kwa mazoea. Siku hizi hakuna Wanawake wanaopenda tabu au kutesa moyo. Ndo maana unaona ndoa nyingi hazidumu.

Mwanamke wa siku hizi akisikia kwamba una mchepuko anakuacha, yaani hajaona just tu kusikia..

Mwanamke wa siku hizi ukimletea mapombepombe yako wakati yeye hanywi na akikukataza ukakataa unaachwa, bora uoe mnywaji.

Mwanamke akiongea muache aongee hadi hasira ziishe, huwezi mshinda kwenye kuongea hata ukimeza spika. Mwanamke akiongea ukamjibu utaishia kugombana naye halafu kesho anakuacha anarudi kwako anasema ulimpiga hata kama umemfinya tu.

Usitake kushindana na mwanamke, ukiona umeanza kushindana na mwanamke, jijue ndoa yako imeanza kuteteleka kesho yake anakuacha unabaki unashindana na baridi usiku na akiondoka unabaki unashindana na kubadilisha wasichana.

Mkeo mheshimu na umnyenyekee vinginevyo utaachwa.

Watoto wadogo watabisha lakini huu ni ushauri nawapa kutokana na experience.

Usiguse simu ya mkeo, bila ruhusa yake ukiigusa utaipasua then mtagombana atakuacha.

Umeoa mwanamke mwenye mtoto au watoto ukataka kumfuatilia anapompeleka mtoto kwa baba yake jua utakufa kwa presha kukonda kwa wivu maana yake utaachwa. Siku ukiwafumania utaambiwa alikutangulia kuniona then unaachwa.

Kama unamhitaji mkeo au unampenda na unataka kufanya naye maisha usimfuatilie.. Muache Mungu amuongoze, wewe Mwanaume dumu magotini mwa Mungu akiomba akusaidie, hakika utashinda.

Walioshindwa na ndoa au walioachika wataanza kusema amekupa limbwata.. Usijali maneno yao sababu ukiachwa watajisifia sana.

Usipofuata huu ushauri jua kesho unaachwa.

Kama huogopi kuachwa jua hujawa tayari kuwa na familia. Usoe na endelea na ubazazi, kama umeoa acha kumtesa mtoto wa watu.

Kama unaogopa kuachwa basi oa na tembea katika misingi hii upate wa kukuzika na kukulilia siku ukifa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post