WAKATI MWINGINE DADA ZANGU SIWAELEWI;


Unajua kabisa kuwa wewe ni mkristo, unatoka katika familia ambazo hata wakisikia jina la kiisalamu wanachanganyikiwa, yaani wanakemea kabisa, lakini unatongozwa na muisalamu, ambaye unaona kabisa kuwa kwao nao hawezi kubadilisha dini, unamkubali, mnaingia kwenye mahusiano, unampeleka kwenu wanamkataa, anakupeleka kwao wanakukataa badala ya kuendelea na maisha yako unaamua kubeba mimba yake?
: halafu baadaye unakataliwa unaanza kulalamika!
Dini ina nguvu kubwa sana katika jamii zetu, inahitaji mwanaume imara sana na mwanamke mwenye msimamo ambao hawajali ndugu ili kuruka kiunzi hiki cha dini. Binafsi naamini watu wanapaswa kufanya kile wanachokitaka na si kile amabcho wazazi wanakitaka.
Lakini swali linakuja je wewe unaweza kwenda kinyume na wazazi wako? Wakikataa usiolewe na dini nyingine je uko tayari kusema kuwa haya ni maisha yangu hayawahusu? Lakini tuchukulie wewe unaweza kusema hivyo, una huo ujasiri, swali linakuja je huyo mwanaume wako anaweza kusema poteli ya mbali, sijali cha ndugu wala nani, sisi tunapendana na inatosha? Kama hawezi unaona hana msimamo msimamo jitoe kwani utaishia kuzalishwa na ndoa utasikia kwenye magazeti ya asubuhi!

Image may contain: 5 people, people standing and wedding


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post