Vijana Shitukeni , Wabongo wanaua watu kwa Makusudi na HIV!!!

Wakuu nachotaka kukihimiza hapa, Watu kua makini, kuzipenda afya zao. Kua waaminifu., matumizi sahihi ya Kondom na KUPIMA KABLA YA YOTE.

Ukisikia Fulan ana Maambukizi ya VVU ,mara nyingi watu huchukulia poa tu ,sababu hayajawakuta wao. Ila ninachoweza kuwakikishieni ni Kua Hamna watu wanaopata Tabu sana kama hawa wanaogundulika kua na Maambukizi, nguvu ya dawa, kunywa madawa kila siku na siku zote za maisha yako. Mnyanyapao wandani mwako na ule wa jamii , na kuyatizama maisha vile ulivyotaka yawe UNAJIKUTA UNAKUFA MAPEMA.


Nmekua nashuhudia Case nyingi sana, wakat fulan najikuta mpaka naumia Ni kwann nilichagua Taaluma hii, na kinachoniumiza ni vile napokua naletewa majibu ya Vipimo toka kwa wateja wangu nakukuta Damu zao hazipo salama na ukitazima umri ni miaka 18-35

Story ni hii... Leo nikiwa Ofisin, alikuja Mdada miaka (mtu mzima ) mzuri waumbo na sura., na msomi . Nikamsikiliza kisha nakamtuma Maabara , Majibu yake akapatikana na VVU . ( Alianguka. Akaishiwa nguvu ) baada ya kurudi sawa, nikaamua kumchukua Historia ndogo.,, akadai Ameolewa, , alomuoa alikua ni MUME WA MTU, aliachana na Mkewe, ktk kuhoji zaidi, Nikagundua Mwanaume alonitajia pia ni Mteja wa hapa hosp kwetu wa CTC.

Nkashtuka, Nkahoji na Jina la mwanamke wake alimfukuza, kunitaji naye ni Mteja wetu wa hapa wa mwaka mmoja nyuma, ila siku izi haonekani.



Sasa hilo ni dogo, Kumbe baada ya kuachana
Mama huyu ( Mteja wetu wa zaman) kaenda kuolewa upya na Jamaa mwingine.

Baba huyu naye ndo akaamua kumuoa binti huyu mzur ,msomi nahatimaye kamuunguza.


Vijana wa kiume ,Jalin afya zenu. Penden afya zenu , kondom na kupima na kua waaminifu ndio nguzo imara ya usalama wa Damu . USIMWAMIN MTU KABISA SABABU TU AMENENEPA. AMENAWIRI, ANAONGEA KWA KUJIAMINI.

Vijana wa Kike, Msipende ndoa sana, msipende wepesi wa maisha, msipende kujirahisisha hata kufikia hatua ya KUSAHAU UTHAMANI WA MWILI NA ROHO YAKO NAKWAMBA DUNIA BADO INAITAJI MCHANGO WAKO.


Dada huyu alikua na Shape la maana. Mweupe, kajaaa , hips zimekimbiana. Makalio ya haja, na alikua mwenye BASHASHA, FURAHAAA ANACHEKA SANA ,lkn kajikuta anaondoka kainamisha kichwa chini na akijilaani " Ni kwanini alikubali kuolewa najamaa bila kwanza kumpima".

( Sasa sijui nyumban uko leo itakuaje.ila kwa uwezo wetu tumejitahid kumuweka sawa, na akaahidi kuja na mwenzake, na ameanza Matibabu ).



Kwann nmetumia Tukio hili? Kwa sababu waBongo hawaelewi bila mfano.


Kijana unayejua malengo yako tambua kua UKIMWI UPO , NA HATA HUMUHUMU JF WAPO WANAOUA WATU MAKUSUDICALLY !!

The Devil puts a spoonful of honey into neighbor's Wife


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post