Unadhani nawe ni yule ambae hujui hata kwa nini upo kwenye hayo mahusiano?

 Unadhani ni kwa nini unaona mahusiano uliyopo hayana mwelekeo lakini unazidi kuyang'ang'ania?
Unadhani kuna mtu unamkomoa ukiendelea kubaki kwenye hayo mahusiano ambayo yanakuumiza kila siku na kuyajutia?
Mpendwa! Muda ni mali na ukienda haurudi nyuma. Kuna wakati lazima ukubali kwamba umekosea na uanze upya. Natambua leo hii wengi wenu mnaogopa kuanza upya kutokana na sababu mbalimbali.
Sasa leo hii kaa na utafakari baadhi ya mambo kwenye mahusiano yako alafu jitafute pale ulipopotea na amua sasa kuyafanyia kazi mahusiano yako na maisha kiujumla, utaona mafanikio.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post