Umewahi jiuliza upo na Mpenzi/Mwenza wako kwa sababu gani? - EDUSPORTSTZ

Latest

Umewahi jiuliza upo na Mpenzi/Mwenza wako kwa sababu gani?


Upo na MPENZI/MWENZA wako kwa sababu gani?
Kuna msemo “All is fair in love and war” – ni kwa msemo huu ambao unaweza elewa maana yake – maana ingekuwa kila mmoja ana uwezo wa kusoma akili ya mtu wake kujua yupo nae kwa ajili ipi, nadhani ingekuwa balaa zaidi ya faida. Na hili ni kwako pia msomaji… Are you true to yourself? Umewahi jiuliza honestly upo na mpenzi wako kwa sababu ipi/zipi.
Mapenzi ni mchezo wa ajabu saana. Wanadamu hutaka awe na wa karibu wake hasa Mpenzi kwa sababu tu kuwa anapendwa na anapenda pia. Haijalishi mpenzi huyo ni kitu gani kiliwaunganisha na kuwa wapenzi, iwe ni mapenzi ya dhati juu yake, iwe kwa ajili ya hitaji Fulani toka kwake, iwe kwa sababu ya muonekano wake – mwisho wa siku kwa wale waliopo katika mahusiano ya muda mrefu hujifunza na hatimaye kutambua kuwa mapenzi ni kiungo kimoja wapo tu cha viuongo vingi vya kuwa katika mahusiano na mtu wako huyo. Kuna viungo vingine huwepo na  pengine kuwa hata na nguvu zaidi kuliko hata kiungo cha ‘Penzi’ katika mahusiano hayo.
Mapenzi ni muhimu katika mahusiano, ila bado nafasi yake ni ndogo ukifananisha na viungo vingine. Mahusiano siku zote suala si kuangalia Mapenzi tu sababu pamoja na kuwa mapenzi ni muhimu bado yana nafasi ndogo tu katika kujenga mahusiano thabiti yaliyojaa furaha na amani. Unaweza usiwe umempenda kwa dhati mtu wako ila ukaridhika na kumkubali bila kujalisha yupo vipi ama ni wa hali gani; hilo likafanya kuwa na Amani katika mahusiano yenu alimradi na mtu wako awe hivyo pia.  Kuna watu ambao wapo pamoja na hawana mapenzi yale ya dhati na wana amani na furaha tokana na kuheshimiana, kujaliana na kuthaminiana, na hali hapo hapo kuna wale ambao wana mapenzi ya dhati na mapenzi yao yana matatizo mazito ambayo wanashindwa kabisa kuyaweka sawa kwa wao kuwa na amani katika penzi lao hilo.
Kwa muktadha huo, haiepukiki kuwa na sababu mbali mbali ambazo huwafanya watu kuwa na watu waliowachagua kuwa nao katika mahusiano. Mapenzi ikiwa moja ya sababu ya  baadhi kuwa katika mahusiano, bado kuna sababu nyingine nyingi ambazo huwa ni sababu za msingi kwa baadhi kuwa na wapenzi wao. Hivyo sababu za kila mmoja kuwa katika mahusiano zimetofautiana from couple to couple na mara nyingi hata mtu na mpenzi wake pia.
Baada ya kusoma hapa, ni vema ukajiuliza ndani ya nafsi yako upo na mpenzi wako kwa ajili ipi, ukipata jibu na kusoma haya yanayofuata utakuta linaweza kuwa limegusiwa hapa, or ikawa pia kuna sababu zingine zaidi ya nilizo ainisha hapa, ukasaidia kutoa mawazo ya kipi kinaongezeka katika sababu hizi hapa.
 UTEGEMEZI
Hii ni kwa wale ambao mara nyingi hana uwezo wa kujitegemea. Na kama ana uwezo wa kuitegemea ni kwa maisha ya kiwango ambacho ni cha chini na asingependa maisha hayo. Hivyo ina maana unakuwa upo  na mpenzi wako sababu yeye ndie anayekuweka mjini, unajuwa kuwa bila yeye maisha yako yatakuwa hayana muelekeo au hata kutokuwa na guaranteed secure future. Saa ingine hata humpendi, ila humchukii na kichwani zipo za kukutosha kutambua kuwa bila yeye huna lolote, mbele wa nyuma. Utegemezi huu upo wa aina mbili;
Utegemezi wa Kiakili (kutokujiamini) – Mtu huyu anakuwa na low self-esteem anahitaji kila mara kuambiwa na kusifa na mtu wake ili yeye kuweza kujiona wa maana.
Utegemezi wa kusaidiwa (kutokujiweza) – Haya maelezo yanajitosheleza mwanzo wa kipengele hiki.
VIHAMASISHI
Hii inatawaliwa zaidi na mazingira – mazingira yanakuwa ndiyo chanzo cha kuwa pamoja. Mfano kufanya kazi pamoja mara nyingi na saa ingine kujikuta katika mazingira ya kuhamasisha sex. Kwa wengine inaweza kuwa kosa la mara moja na wasirudie tena na hali kwa wengine ikawa mwanzo wa mahusiano. Inaweza tokea pia kwa wale ambao ni marafiki wa karibu ambao kila mmoja hufurahia uwepo wa mwenzie tokana na kuwa na mengi ambayo wanagongana kimtazamo, mawazo, misimamo n.k na kisha kujikuta mwisho wa siku mpo katika mahusiano. Kunaweza kuwa na mifano mingi zaidi ya  hii kwa misingi kuwa mazingira hamasishi kwa mahusiano ama ngono ni mengi sana.
INSECURITY
Hujiamini… hujitambui… na wala hujijui bado. Na kama wajua basi huamini utambuzi wako. Unaona kana kwamba huyo mpenzi wako ni your lucky charm, hata kama unafanya kazi na una maendeleo hasa kama uliyapata ukiwa naye unaona kama vile bila yeye haitawezekana kuendelea. Unaona kama vile huwezi mpata mpenzi mwengine aliye bora kama huyo… aidha kimuonekano, ki maisha, ki maslahi, kimaendeleo n.k. Unaona kama vile kuwa nae ni bahati sana lasivyo utampata beneath huyo mtu.
UFAHARI
Hii mara nyingi hutegemea nafasi, jina, wasifu kwa mpenzi wako. Kama vile kuwa na jina kubwa… kazi nzuri… Maisha mazuri… anaheshimika katika jamii… anakubalika na wengi, anatamaniwa na wengi, ana mvuto na mengine kede kede. Mhusika anakuwa si kwamba kampenda mtu wake, ila tu anakuwa kapenda zaidi kuwa jamii itaona yupo nae na kwamba yeye ndiye mwenye bahati ya kuwa nae kama mpenzi wake. Wahusika wa kundi hii huwa katika mahusiano haya kwa sababu ya ‘Ubinafi’. Mfano anaweza akatoka na mtu maarufu ili kupata umaarufu pia wa haraka, anaweza toka na mtu ambae watu huona ni mzuri/mrembo/mtanashati ili tu aonekane kana kwamba yeye ni bora kuliko wote hapo kwa kumpata huyo mtu. Anajua kabisa humpendi ila anakufaa kuwa mpenzi wako katika macho ya jamii.
KUKATA TAMAA
Hili ni sana kwa wale walio hangaika sana katika ulimwengu wa mapenz. Kila ampatae tokana ma viwango vya aina ya watu ambao anavutiwa nao (saa ingine bila hata viwango hivyo) mwisho wa siku anaumizwa. Kila mpenzi ambae kawahi mpata amemtenda na kumuumiza moyo, mwisho wa siku anapata mtu ambae walau ana mwelekeo na ingawa ana madhaifu ila ni ya kibinadamu hivyo huona ni kheri aridhie na kutulia kwa huyo mtu kuliko kuendelea kutendwa tena.  Anakuta toka awe na huyo mtu kapata uhafueni sana, hivyo inatokea anaridhika hivyo hivyo hata kama si ambae angependa kuwa nae.
GUNDI ASILIA YA NDOA
Hii ipo sana kwa wale ambao ni wanandoa; yaani mtu na mwenza wake.. wamejijenga pamoja. Wana watoto, rasilimali na maisha yao yapo so tangled pamoja tayari. Lile wazo ama kitendo cha kutengana ni kuyavuruga kabisa maisha kwa kiasi kikubwa sana. Mara nyingi watoto na mali ndiyo force kubwa. Wanandoa wote wanaweza tambua kuwa hawapendani kabisa wapo radhi hata wahame vyumba kila mmoja awe na chake (hata kama kitanda) lakini mwisho wa siku wanaheshimiana, mbele ya jamii wanajulikana kama mtu na mkewe huku ndani haviivi kabisa.
KULAZIMISHWA
Aidha ulilazimishwa kuwa nae… au unaweza kuta ni wa kurithi. Kuna kabila na mila ambazo hadi leo inatakiwa utafutiwe mtu wa kuoana nae… labda katika ukoo ama kwa wakaribu wa familia. For instance dada kaolewa kazaa watoto wawili then anafariki na soln inaonekana ni bora aolewe mdogo wa marehemu. OR kaka anafariki then kaka ama mdog wa marehemu anaoa mke wa marehemu kwa njia na nia ya kurithi.
COMPATIBILITY
Hampendani, ila heshima kwa saana. Wote mmeweza na kufaulu katika ku compromise. Yale ambayo mwenzio hapendi umeweza epusha na wala hujaona tofauti yoyote with the justification kuwa sio ya msingi sana kuendelea na vivo hivo kwa mwenzio. Mmekutana tabia, maybe wote ni wacheshi/wapole, wote hupenda privacy yake mwenyewe na huheshimu ya mwenzie… vitu kama kufuatiliana, kuchunguzana, kushikiana simu, kupelelezana au kuchokonoana hakupo. Watu hawa mmoja wapo anaposafiri akakaa huko hata kwa kipindi kirefu mawazo kama kusalitiana hata hayawatembelei kichwani kwao (hata kama kweli wanafanya); hawa complicate maisha, kama hawapo pamoja simu mara moja or mbili kwa siku… more out of obligation than love. Hawa mmoja wao hata awe na mpenzi mwengine anajua kabisa hawezi kuwa as perfect as huyo alokuwa committed kwake.
MAPENZI YA DHATI
Hapa ni kwa wale wenye mapenzi ya kweli, wale ambao kama mioyo yao ni dhaifu huweza kujiua na kuua kabisa katka jina la ‘Penzi’. Anaona bila huyo mtu wake hakuna mwingine hapa duniani hata umwambie nini, hata umshawishi nini na hata utumie jitihada gani! Hapa ndipo pale msemo wa “Hakunaga’ unajitosheleza kabisa.
Ni kwa misingi hiyo kupenda kwa dhati kunaweza fanana toka mmoja na mwingie ila mwisho wa siku kila utakae mwambia akueleze nini maana ya mapenzi kila mmoja atakupa jibu lake. Maelezo tofauti kabisa ila mwisho wa siku yote yakibeba uzito wa jinsi gani mtu fulani katika maisha yake humfanya ajisikie raha, ajisikie tofauti, ajisikie wa pekee, ajisikie vyovyote vile katika muelekeo war aha zote zilizopo hapa duniani…
Ubaya tu wa haya mahusiano, ni rahisi sana kutodumu, ingawa kuna wale wenye bahati huwa yanadumu, na kuna wale wenye bahati tokana na ubinadamu, mtabadilika, mapenzi yatapungua ila mwisho wa siku yatarudi katika mstari.
Mwisho napenda niongezee sababu kawaida si moja, sababu inaweza kuwa zaidi ya moja – ingawa sababu moja hubeba uzito kuliko sababu zingine ambazo zipo. Lakini vyovyote iwavyo, pendaneni, thaminianeni, heshimianeni na jengeni mahusiano kujenga Amani na furaha kati yenu…
 Usikose kukutana namimi katka makala ijayo….




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz