Ukiunganisha matukio ambayo mwenza wako anakufanyia basi unaweza ukapata jibu la kwamba unapendwa au hupendwi.


Kuna vihoja vingine unafanyiwa yaani kabisa unaona hizo ni dalili za upendo kufa au kwamba mwenza wako hathamini kabisa kujitoa kwako. Ukitazama kwa makini baadhi ya mahusiano basi utagundua yamebaki jina tuu lakini mioyoni mwa wawili hao basi hakuna tena upendo wa dhati.
Inafika wakati unaona kabisa unajilazimisha na ukweli ni kwamba hutakiwi tena kuwepo hapo kwenye hayo mahusiano.
Ndugu mpendwa! Maisha ya mahusiano sio ya kulazimishana au kutumia nguvu. Maisha ya mahusiano ni hiari ya mtu na jifunze kupenda pale ambapo unaipata amani ya moyo pamoja na furaha.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post