Ukiona uliyenaye kwenye mahusiano hazungumzii chochote kuhusu kesho yenu jua wazi yuko nawe kwa sababu penzi lenu ni la leo tu.

Ukiona uliyenaye kwenye mahusiano hazungumzii chochote kuhusu kesho yenu jua wazi yuko nawe kwa sababu penzi lenu ni la leo tu.
Mwanamke hebu ifike wakati uache kuhangaika na mahusiano na uangalie furaha yako kwanza. Nazungumza na wewe mwanamke ambae kila ukiingia kwenye mahusiano umekuwa ukiumizwa na kusalitiwa.
Usipoitafuta furaha yako kwanza basi kila siku utashawishika kuingia mapenzini sababu ya kwenda kuitafuta furaha na sababu utakuwa na mategemeo makubwa utataka huyo mwanaume awe mkamilifu kitu ambacho hakiwezekani hivyo utaona hakuridhishi.
Tulia kwanza mpendwa! Jitafute ulipopotea na ulipokosea kisha jifunze kutokana na makosa. Hata kama huyo mwanaume mliyeachana ndo mwenye makosa usiendelee kumlalamikia na kumlaumu bali jitazame wewe mwenyewe na jitafakari kwa makini wapi ulipotoka na wapi unapoelekea.
Ukifika muda sahihi na kujiona upo sawa na unaona kuna mtu ambae nae yupo tayari kuwa nawe na ana sifa na vigezo basi unaweza kuingia tena mapenzini.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post