Mara nyingi mwanaume akishampata mwanamke huanza kuhisi kama hamhitaji tena, hahitaji kumfanyia mambo yale amabyo alikua akimfanyia kabla ya kumtongoza. Anaona amefika hivyo kuamua kuabdilika, kuwa kiburi na kuwaza haendi popote. Labda nikuambie kitu kimoja, unaweza kuona kama haendi popote lakini wanawake ni wavumilivu sana, atavumilia kila kitu, atajaribu kila kitu lakini mwanamke akikuchoka anaweza hata kukuwekea sumu ili kuwa huru kutoka katika mikono yako.
Ninachomaanisha hapa nikuwa, mwanamke akikuchoka ataondoka tu, atatafuta mlango wa kutokea na hatageuka nyuma, unaweza kuwaza hata akiondoka si natafuta mwingine, kwanza wanawake wako wengi. Ndiyo ni rahisi sana kutafuta mwingine, wako wengi kuliko sisi, lakini ni vigumu sana kupata ambaye atakupenda, ambaye atakuthamini, unaweza kujikuta unakua mtu wa kutoka mwanamke mmoja kwenda mwingine.
Utaona raha mwanzoini lakini kuna kitu kinaitwa umri, hiki huongozana na ndugu yake amabye anaitwa majukumu. Hawa watu wakikaa pamoja na wakianza kukusumbua basi hata ukiletewa wanawake mia ukawekewa mbele yako hutawatamani kwani akili itakua imechakaa. Ndiyo baada ya muda ujana utaisha, wale marafiki wa kuongozana nao kula bata watakua washakua watu wazima wanakukwepa kwakua huna uelekeo.
Sasa kuna mtu anaitwa majukumu atakuganda na hutaamini, una watoto sita wote Mama tofauti tofauti, mwanzoni si ngumu sana lakini wakishaanza shule utajikuta unafanya kazi kama chizi na watakuchanganya. Sasa si utasema nawaachia Mama zao, uwe tu na bahati ya kukutana na Mama ambaye anajua kulea, kama nayeye ni umiza kichwa basi utachanganyikiwa. Lakini hata kama utakutana na anayejua kulea ndugu yangu utajiona fala wanao kulelewa na wanaume wengine.
Ndiyo pamoja na huyo mwanamke kufanya kazi lakini kuna mwanaume mwingine analea, inaweza isiwe moja kwa moja lakini kama ananunuliwa nguo na mwanaume mwingine basi ile hela ya nguo ndiyo anatumia kulea wanao. Ndiyo umri nao utakua haukuachi, utazeeka huna uelekeo, umeamua kutulia watoto wakubwa hawakutaki kwakua uliwatelekeza, sasa wale wadogo uliozaa na mke mpya ambaye umaemua kutulia naye ni umiza kichwa.
Una miaka 55 lakini mtoto wa ndani ya ndoa wa kwanza basi hajaacha kuvaa Pampas. Yes nirahisi kumaucha mwanamke anayekupenda lakini kuishi bila yeye ni vigumu kuliko unavyodhani hivyo kabla ya kujifanya kidume na kuanza kudhalilisha wanawake hembu jiulize je nataka kuishi maisha ya aina gani? Kama unataka kuwa mwanaume mwenye furaha na mwenye mafanikio tafuta mwanamke ambaye mtatengeneza maisha na mheshimu!
MIMI NISHAMALIZA KAMA IMEKUGUSA SOMA KIMYAKIMYA
Post a Comment