πŸ’• SIRI ZA KUDUMISHA PENZI LISITETEREKEπŸ’ πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯ - EDUSPORTSTZ

Latest

πŸ’• SIRI ZA KUDUMISHA PENZI LISITETEREKEπŸ’ πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯

πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•


Jifunze lugha tano za mapenzi - Mwananchi

UNAWEZA kuanzisha kitu chochote, wakati wowote lakini jambo la msingi zaidi ni namna ya kudumisha na kuendeleza ulichokianzisha. Kwa mfano, unaweza kufungua biashara fulani lakini ukafeli katika kuisimamia na kufuja fedha, hutafanikiwa!, ndivyo ilivyo hata kwenye uhusiano. Unaanzisha sawa, lakini vipi kuhusu kudumisha penzi lako likaendelea kuwa na nguvu zaidi siku hadi siku?
πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•
TAMBUA THAMANI
jithamini kwanza na kumuona mwenzi wako ni wa muhimu kwako,na uone ni mtu speacial kwako ndio utaweza kudumisha penzi lako milele na milele
πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•
MHESHIMU
Mwanaume anapenda sana kuheshimiwa na mpenzi wake. Kwa kawaida, mwanaume akigundua haheshimiwi au unafanya hivyo kwa kumridhisha tu na si kutoka moyoni, ni rahisi kukuacha.
Kama kichwa cha familia, lazima apewe nafasi ya kutoa uamuzi tangu mapema. Ikiwa utakuwa na majibu mabaya kwake, huonyeshi heshima ni wazi kwamba atakuacha mapema, maana utakuwa umepoteza sifa za kuwa mama wa familia.
πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•
KUWA MFARIJI WAKE
Siku hazifanani, hivyo inawezekana kabisa siku moja mwenzi akawa na matatizo aidha ya kiakili, kimaisha au kikazi. Ikitokea umegundua mpenzi wako ana matatizo na hana furaha, wewe ndiyo unatakiwa kuwa mfariji wake.
Lazima umsome, ujue yukoje ili iwe rahisi kugundua tofauti atakayokuwa nayo siku akiwa hayupo sawa. Kumfariji ni jukumu lako, utakuwa umeonesha uwezo wako kikamilifu wa kuwa mama bora hapo baadaye.
Mama ambaye anaweza kurudisha amani ya mume wake, pindi inapokuwa mashakani. Ni mambo yanayowezekana kabisa . Lazima ujipe umuhimu kwa mwenzako. Akikaa afikirie na kuona kuwa kweli wewe ni muhimu katika maisha yake.
Aone kuna ulazima wa kuharakia ndoa mapema kwa sababu utakuwa umemjengea imani ya moja kwa moja. Huo ndiyo ukweli . Ikiwa kinyume cha hapo, ni kwamba utakuwa unajiondoa mwenyewe kwenye sifa ya kuwa mke sahihi.
πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•
KAULI
Inakupasa uwe na ulimi mtamu. Simaanishi uuweke sukari ili uwe mtamu; hapa nazungumzia juu ya kauli njema. Hutakiwi kuwa na majibu ya hovyo kwa mwenzako, uzungumze kwa staha na heshima. Hapo utakuwa unaingia moja kwa moja kwenye nafasi ya kuwa mke.
Wale wa mitaani, wanasikiliza maneno ya hovyo kutoka kwa marafiki zao ndiyo wanaoweza kuwa na lugha chafu kwa wenzao. Kauli mbaya hukuondolea sifa ya ustaarabu na moja kwa moja unajiweka pembeni mwenyewe. Nani atapenda kuwa na mtu ambaye hajiheshimu? Ana majibu mabaya? Hajali kinachotoka kinywani mwake? Ni nani?
πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•πŸ’•
ACHANA NA MAKUNDI
Mwanamke mwenye staha hafungamani na makundi ya mashangingi wa mjini. Wanaume hasa wanaotaka kuoa, hawapendi mke mtarajiwa awe shangingi au anayejihusisha na wanawake wa aina hiyo.
Inaaminika kwamba kwenye makundi hayo hujadiliwa mambo yasiyofaa ndiyo maana wanaume wengi hawapendi wanawake wenye tabia za kukaa kwenye makundi ya mashangingi. Chukua hii kwa faida yako.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz