Sio kila mtu anaeku-treat vizuri anastahili nafasi katika moyo wako. Baadhi ya watu ni mbwa mwitu waliojivika ngozi ya kondoo, na wako vizuri sana katika mikakati yao.
Hivyo, kuwa makini sana na watu unaowakaribisha moyoni mwako. Usiwe na haraka ya kuamini watu. Usiharakishe kufanya vitu ambavyo utakuja kuvijutia punde kidogo. Chukua muda wa kutosha kumjua mtu kuhusu interest yake, tabia yake, malengo yake kuhusu wewe na mahusiano yenu.
Kama mtu anakung'ang'aniza kuharakisha jambo ambalo kwalo, wewe hauko tayari au hauko comfortable nalo, hiyo iwe alama ya mapema kwamba, wako kwa muda tu na sio lifetime commitment.
Kuwa makini sana na watu na jifunze kuepuka mambo yatakayokuletea majuto mbeleni. Maisha ni zawadi tuliyotunukiwa na MUNGU, si sawa kwa wewe kuendelea kuwa mtu wa kuumia, kuwa disappointed na stress kibao mara kwa mara. Unatakiwa ujifunze kupitia makosa, na kulitumia funzo ulilopata.
Maisha yako ni bora na yenye thamani kubwa sana, furaha na amani ya moyo ndio chachu ya kufanikisha kusudio la uwepo wako.
Licha ya maumivu tunayosababishiwa na wale tuliowaamini, tusichoke! tujifunze kujithamini na kufurahia maisha yetu Pasina kutamani maisha ya wengine, maana, hatufahamu na wao wanapitia magumu yepi.
Post a Comment