Na. Brayton official
Kila nikikumbuka nashindwa hata kulia, nimejaribu kujiua zaidi ya mara tano lakini ilishindikana, sasa hivi naamini Mungu anataka niishi na nimeamua kupiga moyo konde ili niendelee na maisha kwani kama nipo hai leo basi naamini Mungu ana sababu zake.
Kila nikikumbuka nashindwa hata kulia, nimejaribu kujiua zaidi ya mara tano lakini ilishindikana, sasa hivi naamini Mungu anataka niishi na nimeamua kupiga moyo konde ili niendelee na maisha kwani kama nipo hai leo basi naamini Mungu ana sababu zake.
Habari Kaka Brayton Offical Love; nimeanza hivyo kwakua nilishakata tamaa ya maisha kutokana na mapenzi lakini kutokana na makala zako sasa hivi nina matumaini tena, nnimeamua kuweka maumivu pembeni na aibu pembeni.
Mimi ni Binti wa miaka 30, sijaolewa lakini miaka mitatu iliyopita nilifunga ndoa ya kiislamu lakini mume wangu alinipa talaka tatu siku hiyo hiyo ya harusi, yaani ndoa tulifunga asubuhi akanipa talaka saa nne usiku siku hiyo hiyo ya harusi.
Nimeamua kundika kisa changu Kaka kwasababu umeniponya, umenipa matumaini mapya na nataka wanawake wenzangu kujigunza kutokana na ujinga wangu. Kuna mambo mengi ambayo wanawake tunayafanya kwaajili ya kukomoa watu wengine lakini yanakuja kutugeukia huko baadaye.
******
Kwakifupi nikuwa wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilipata Baba mmoja, mtu mkubwa tu serikalini, sasa kama unavyojua wanaume watu wazima wanavyojua kuhonga, alikua akinihudumia kwa kila kitu, alinipangia chumba na kunilipia ada.
Kwakifupi nikuwa wakati niko chuo mwaka wa kwanza nilipata Baba mmoja, mtu mkubwa tu serikalini, sasa kama unavyojua wanaume watu wazima wanavyojua kuhonga, alikua akinihudumia kwa kila kitu, alinipangia chumba na kunilipia ada.
Mwanzoni nilimuambia nampenda lakini amheshimu mke wake, mambo yalivyoendelea nikapata kiburi cha pesa tukaacha kufanya kificho tukawa tunatoka dhahiri. Lakini yule mwanaume nilimuweka kiganjani hivyo nilikua namuendesha.
Zamani alikua hataki nimpigie wakati akiwa na mkewe, lakini wivu ukanijaa hivyo nikajikuta nampigia wakati wowote na kwakua nilishamuweka kiganjani alikua anapokea simu hata mbele ya mkewe.
Siku hiyo mkewe alinipigia simu na kuniomba niachane na mume wake, kusema kweli nilimtukana kama mtoto mdogo, nikimuambia mume ni wakwake akiwa kwake lakini akitoka ni wetu sote.
Lakini Mama wa watu hakuishia hapo alinifuata kabisa, ni Mama mtu mzima karibu kufikia umri wa Mama yangu. sikumjali, sikua tayari kuachana na pesa hivyo nilijikuta naingiwa na shetani nataka hata kumpindua yule Mama.
Sikuishia kupiga simu tu, nilikua natuma mpaka mapicha na vizeo za uchi, namtumia yule mwanaume nikiwa bafuni, nikiwa chumbani, na kila kitu. Sikujali kama mkewe anajua wala nini na nilituma hivyo ili kumkomoa yule Mama kwa kunifuatafuata.
Maisha yaliendelea, nilimazlia chuo na kupata kazi yangu nzuri tu, baada ya kupata kazi nilipata mchumba ambaye ni mfanyakazi mwenzangu hivyo niliachana na yule mzee na kwa bahati nzuri nilipomuambia hakuning’ang’ania sana alinielewa.
Miaka miwili baadaye nilichumbiwa na kuandaliwa harusi kubwa tu. Sherehe ilifana kwani tulikua tunapendana sana, sasa kilichotoke siku ya harusi yangu kilibadilisha maisha yangu kabisa na mpaka leo ninalia na najutia kwnaini nilifanyaujinga ule.
******
Ilikua ni siku ya furaha sana kwangu, lakini iliingia kinyongo wakati wa zawadi, watu wakiwa bado hawajala chakula zawadi zilianza kumiminika huku mziki mkubwa ukipigwa.
Ilikua ni siku ya furaha sana kwangu, lakini iliingia kinyongo wakati wa zawadi, watu wakiwa bado hawajala chakula zawadi zilianza kumiminika huku mziki mkubwa ukipigwa.
Wakati zawadi zinatolewa kama mnafahamu katika ukumbi kunakua na Projectile ambazo huwekwa kwajaili ya kuonyesha picha za matukio ukutani kwa wale walioko mbali. Lakini pia kuna zile CD ambazo huwekwa kwaajili ya kuonyesha picha za zamani za Bwana na Bibi harusi enzi za utoto wao kama historia flani.
Sasa kuna kijana mmoja aliomba kuwekewa CD yake, ilinza kwa mziki, lakini ghafla picha kwenye Projectile ukutani zilibadilika, zilikua ni picha zangu za uchi, zile zile mabazo nilimtumia yule Baba wakati nikiwa chuoni.
Mwanzoni sikujua mpaka niliposikia kelele, ilibidi DJ kuzima harakaharaka lakini alishachelewa kila mtu alikua ameona. Lakini haikuishia hapo simu ya mume wangu iliingia meseji ya whatsapp.
Kulikua na video ambazo pia nilimtumia yule Baba, nikijifanyia mambo ya ajabu ili kumtega. Simu ya Mwenyekiti wa kamati nayo iliingia meseji na baadhi ya ndugu wa upande wa mume wangu, ikiwemo Baba mkwe wangu.
Harusi ilibadilika na kuwa kelele, kila mtu akiongea chake, wakwe zangu walikasirika, mume wangu hakusubiri hata kutoka ukumbini alinipa talaka tatu palepale, akaniacha huku akisema nimemdhalilisha mbele ya ndugu zake na wafanyakazi wenzake.
*****
Hakuna siku ambayo niliwahi kuaibika kama siku ile, watu walimsihi mume wangu lakini wapi, hakusikiliza. Aliondoka kabisa na kuniacha ukumbini, nilijikuta na dondoka na kupoteza fahamu, walinipeleka hospitali.
Hakuna siku ambayo niliwahi kuaibika kama siku ile, watu walimsihi mume wangu lakini wapi, hakusikiliza. Aliondoka kabisa na kuniacha ukumbini, nilijikuta na dondoka na kupoteza fahamu, walinipeleka hospitali.
Lakini haikuishia hapo, kesho yake picha na video zilisambaa Ofisi nzima. Nilikaa ndani wiki tatu nalia tu, nilishindwa hata kwenda kazini kutokana na aibu, nilijaribu kunywa sumu mara tatu lakini zote hizo niliwahiwa na kupona.
Nilijaribu kunjinyonga na hata kujichoma kisu lakini niliokolewa. Kazini niliacha kabisa kazi kwani mbali ya aibu sikutaka kwenda kuonana na mume wangu ambaye wiki mbili baada ya lile tukio alioa mwanamke mwingine.
Sasa hivi naendelee vizuri na namshukuru Mungu kwamba ni watu wachache tu wale wakatribu wanajua kwani haikutumwa sana kwneye mitandao. Nimehama mkoa na sasa nafanyabishara ndogondogo sitaki hata kwenda kuomba kazi sehemu.
Nimeamua kuandika kisa changu kwakua bado kuna wanawake wanatembea na waume za watu na wanawatumia picha za uchi wakidhani kuwa wanawakomoa wake zao. Wanawaona wale wake zao wajinga labda wataziangalia na kuziacha tu.
Ingawa yule Mama kitendo alichonifanyia kilikua cha kinyama lakini simalaumu sana kwani hata mimi niliyomfanyia yalikua ni ya kinyama pia. Bado wanawke wengi tuna ule ujinga kuwa ukishaangalia picha zifute.
Humkomoi mtu yeyote zaidi ya kujidhalilisha kwani hakuna mwanamke atamuacha mumewe wametoka mbali kwasababu ya kimalaya flani kimetuma uchi wake kunuka katika simu yake!
Hivyo badilika, yule ni mkewe na ipo siku atajitambua ataenda kumuomba msamaha na atamsamehe, wewe atakuaibisha na kukuharibia maisha yako yote.
Mimi mpaka sasa hivi naogopa hata kuolewa tena kwani najua kuwa yanaweza kunitokea yaleyale. Hata nisipoolewa harusi vipi akituma picha zangu za uchi ofisini kwa mume wangu, akawatumia marafiki zake.
Mimi nitavumilia aibu, nitazoea lakini je huyo mwanaume atavumilia, vipi wakwe zangu wakaitumiwa watakuaje. Naumia sana na nina wasiwasi sana, ujinga kidogo umeniharibia maisha yangu. usifanye ujinga kama mimi.
Nimejaribu kumuomba msamaha yule Mama lakini anasema sio yeye kafanya vile labda ni wanaume wengine niliokua nawatumia, ukweli sikua na mwanaume mwingine lakini siwezi fanya chochote zaidi ya kulia tu na kumuomba Mungu ampe roho ya imani aisizidi kunishalilisha.
*****MWISHO
JIFUNZE HAPA;
Akina dada wana upumbavu flani anakutumia picha za uchi halafu anakuambia kua ukimaliza kuangalia zifute. Kwanza nikuambie tu ukishatuma picha kwenye mitandao haifutiki tena. Lakini nikuambie kingine hata kama mtu hajui IT lakini nirahisi kupata picha.
Wanaume wengi na watu wengi wakiambiwa futa picha basi hufuta meseji na si picha. Ukiingia kwenye Gallary wala bila kujua IT unakuta picha zote zile, kama huamini hembu jaribu kufuta picha kisha uone itakuaje.
Lakini pia kuna ile sehemu umeweka email yako, na kusema kuwe na backup. Kwamba kila picha na meseji unayotumiwa inaingia kwenye email yako hivyo hata ukifuta kwenye simu na kwenye Gallary ni kazi bure kwenye GOOGLE IPO.
Sasa mtu akiwa na passwed tu anaweza ifungua na kuzipata, sasa jamaa anaweza kukuambia kua mke wangu haangalii meseji zangu, ukamuamini ukafikiri huyo mwanamke ni mijinga kiasi hicho asiangalie.
Anaangalia, anachungulia na ana paswed zote hivyo kabla ya kutuma picha tena unatumia mume wa mtu ambaye mkewe anateseka analia kila siku waza je zikisambaa utapata faida gani? Mume ataomba msamaha atasamehewa lakini wewe/
NIMAMALIZA hambu share maana kuna wanawake wapumbavu wengi tu ambao bado wanamaini kumtumia mwanaume picha za uchi ni kumteka wakati akigoogle tu anakutana na vitu vimeeditiwa kabisa.
Hata kama si mume wa mtu ni boyfriend unajuaje kua hana mchepuko au njia kuu ikaona na ikazichukua na mihasira yake ikasambaza. Amka acha kutengeneza sumu ambayo unaweza kuiepuka, kama hujaweza kumteka kitadai huwezi kumteka kwenye simu.
*****#SHARE
Wanawake wengi hawana furaha kwasababu wanatumia muda mwingi kuwaza kuwa watu watanielewaje. Anabaki kwenye ndoa ya mateso si kwasababu anampenda huyo mwanaume lakini kwakua anawaza nikiondoka jamii itanielewaje?
Anakumbatia marafiki wa kupuuzi ambao humpotezea muda wake kwakua anaogopa kuonekana kuwa anaringa. Anavumilia matusi ya wakwe zake kwakua anaogopa kua akinyanyua mdomo watu watamuelewaje!
Yaani kuna mambo kibao ya kipuuzi ambayo wanawake hufanya kwaajili ya jamii, huumia kwaajili ya jamii, kana kwamba wakifa watakufa na jamii zao! Hembu badiklika amua kua na furaha na kama unateseka teseka kwakuaunapenda mateso na si kwakua jamii itakuonaje!
Post a Comment