Soma kisa hiki kifupi
MKE: Naomba nilipe hela ninayokudai
MUME: Hela ipi mke wangu unayonidai?
MKE: Wiki iliyopita nilitumia hela yangu kumnunulia Sara madaftari, halafu juzi Rama alikuwa anaumwa nikamnunulia dawa kwa hela yangu, halafu wiki nzima mboga nimenunua kwa hela yangu. Hukuniachia hela yoyote uliposafiri kwenda kazini. Jumla nakudai 2,2500. (Elfu 22 na 500)
MUME: OK, kwani Rama na Sara ni watoto wa nani?
MKE: Ni wangu mimi na wewe.
MUME: Kwahiyo, uliwauzia huduma ulizowapa mpaka nikulipe?
MKE: Hapana, lakini nilitumia hela yangu binafsi, nilipe mimi bwana
MUME: Nitakulipa, ila nikifa naacha wosia watoto wakalelewe kwa mama yangu mzazi.
MKE: Kwanini wakati nipo?.
MUME: Kwa kuwa utatumia hela yako kuwahudumia halafu utaanza kuwadai kwa vile huwahudumii bure bali ni biashara. Halafu mke wangu hivi mimi hela nazotafuta ni za kwangu au ni za mimi na wewe na watoto? Hizo zawadi nilizowaletea wewe na watoto utanilipa kwa kuwa nimetumia hela yangu?
MKE: Lakini hela hiyo nili....
MUME: Wewe ni msaidizi wangu, ubavu wangu. Chako ni chetu, changu ni chetu. Nikikulipa tafsiri yake wewe ni mfanyakazi au hawara na si mke. Au una mume wa kumsaidia kutunza familia zaidi yangu?
MKE: Nipe hela yangu Baba Sara, la sivyo utajuta.
MUME: Na wewe lipa kodi ya nyumba yangu, la sivyo ondoka.
FUNZO
Kuoa mke mwenye kazi au biashara usifikirie kuwa atakupunguzia majukum ya familia. Kutoa ni moyo wa mtu. Sio kila mwanamke ana anajitoa kuijenga familia yake.
Wana Ndoa mupo kwa a jili ya kusaidiana na sio kukomoana..
Kuitwa MuMe haimanishi kuwa kila mara yeye ndo ahudumie famiilia..
Kuna mda unakuta MKE ana kipato kizuri huenda kuliko hata MUMe lakin hawez kununua hata chumvi kisa yeye Kaolewa hilo ni jukum la mume
Mambo madogo kama haya ndiyo yanayo vuruga ndoa nyingi sana siku hizi...Ni kuwa makin na sio kuongozwa na ushaur mbovu ..
Pia MUME sio vyema kumuachia MKEo majukum yote ya familia kisa ana kaz au biashara...
Kumbuka Uli muoa yeye na sio kaz yake...Haiwezekan mama ndo awe ana hangaika na watoto mambo ya shule afu baba upo tu na pombe au wanawake wengine
Ichukue
Post a Comment