NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUACHANA NA MTU ULIYEKUA UKIMPENDA/BADO UNAMPENDA!

JINSI YA KUMJUA MPENZI LAGHAI NA MUONGO
 Katika mapenzi hakuna wakati mgumu kama kuachana na mtu ambaye bado unampenda, hasa kama mlitumia muda mrefu kutengeneza mahusiano yenu na mlikua na mipango mingi ya kimaendeleo ya pamoja.

Anaweza kuwa ni mume wako, mke wako au mpenzi wa kawaida tu ambaye ulishazoeana naye. Kuna mambo mengi ambayo mliyafanya pamoja na kila wakati ukiyakumbuka yanakuumiza hasa kama wewe ndiyo uliachwa au mmeachana kwa sababu ambazo ziko nnje ya uwezo wenu (ilikua ni lazima muachane).

Bila kujali sababu za kuachana kwenu, ile kuachana tu mkiwa bado mnapendana au wewe ukiwa bado unampenda nichangamoto kubwa. Nikipindi kigumu cha maumivu, vilio na baadhi ya watu hufikia hata kujiua.

Katika kutambua ugumu ambao watu wengi hupitia katika kipindi hiki nimekuandalia njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kupunguza maumivu na kubwa kabisa kufanya maisha yaendelee.

Hapa nikimaanisha kuwa ingawa huwezi kuyaepuka mumivu moja kwa moja lakini njia hizi zitakusaidia kuamka tena na kujua namna ya kuanza kuwa na furaha tena. Zitakuamsha upya na kukufanya uweze kujiandaa vizuri na mahusiano yanayofuatia kwani maisha ni lazima yaendelee.

(1) Relax, Pumua, Jijali;

Nadhani hiki ndiyo kitu cha kwanza kabisa unachopaswa kukifanya, upe mwili wako nafasi ya kupumua na kupata hewa nzuri. Jijali hakikisha uko sawa kwanza, tafuta sehemu nzuri yenye upepo, kaa, pumua, jinyooshe nyooshe viungo na tuliza akili.

Unaweza kuona kama ni kitu kidogo lakini kupumua kunasababisha mwili kuondoa stress, ubongo kufanya kazi vizuri. Jijali hakikisha unakula vizuri. Ujali mwili wako na hii itakusaidia katika kufanya maamuzi mazuri baadaye, tulia.

Usikurupuke na kuanza kuwaza namna ya kurudiana naye, namna ya kumkomoa, namna ya kumharibia mpenzi wake mpya au namna ya kulipa kisasi. Hapa anza kujiwaza wewe kwanza, safisha akili yako kuhusu yeye na ingiza wewe.

(2) Acha Kujilaumu

Mara nyingi watu baada ya kuachana kuna maswali yanakuja kichwani, hata kama uliyeachana naye ndiyo mwenye kosa lakini akili yako itajilazimisha kujilaumu wewe. Labda alichepuka, utaanza kuwaza labda wewe ndiyo ulikuwa humtimizii mahitaji yake ya kimwili vizuri ndiyo maana akachepuka.

Lakini inawezekana kosa ni lako kweli, kama yameisha yameisha tu na huu si wakati wa kujilaumu. Misingizie Mungu kila kitu kwamba ni mipango yake na jipe moyo kwani kuna kubwa linakuja, acha kujilaumu na acha kufikiri kwamba labda ungefanya mambo tofauti labda msingeachana.

Labda nikueleze tu kuwa hata kama ungefanyaje ni suala la wakati tu kama mmeachana sasa basi mngeweza kuachana wakati mwingine. Huyo sio mtu uliyepangiwa na makosa (kama ni wewe uliyoyafanya) yengeweza kusameheka lakini kwakua si mtu wako ndiyo maana hamko pamoja.

Acha kujilaumu, acha kuangalia mapungufu yako, acha kuangalia madhaifu yako, huu si wakati wa kujifunza kutokana na makosa, utajifunza utakapotaka kuanzisha uhusiano mpya lakini si punde tu baada ya kuachana. Huu ni wakati wa kutuliza akili na kusema hakuna kitu ambacho ungekifanya kikambakiza.

(3) Usijibu Mashambulizi

Wakati mwingi kuachana katika mapenzi kunakuwa sio kwa kistaarabu, inawezekana amekusaliti au wewe ndiyo umekosa na kakuacha kwa matusi. Mmeachana lakini bado hataki kukuacha anakutukana na kila nafasi anayopata basi anakutukana na kukushutumu.

Hiyo kwake ni kama njia ya kujifariji na kutaka kukufanya wewe ujisikie vibaya, lakini kiuhalisia haimsaidii kwani anavyokutukana anazidi kukutaja na kukukumbuka. Kwa maana hiyo basi njia rahisi ya wewe kupona haraka ni kutokumjibu.

Usijibu mashambulizi, muache aendelee na mambo yake na wewe endelea na yako, muache akutukane, akushambulie nak ila kitu lakini kaa kimya. Lakini si lazima umsikilize, kwamba upokee simu zake ili akutukane, hapana kama kuna njia ya kumkwepa basi mkwepe lakini usimjibu.

Muache atoe madukuduku yake lakini ukiona anavuka mipaka basi unaweza ku mblock ili asizidi kukupotezea muda. Ukimjibu na mkawa mnajibishana basi hamtafika mwisho, wote mtaendelea kujiumiza na itakuwa ngumu sana kwako kumsahau na kuendelea na maisha yako.

(4) Usifanye Maamuzi ya Haraka;

Hakuna kipindi kibovu cha kufanya maamuzi kama kipindi hiki hasa maamuzi ya kimapenzi. Inawezekana kakuacha kwa dharau na wewe unataka kulipiza kisasi kumuonyesha kuwa unaweza kupata mwingine zaidi yake na kuwa na furaha bila yeye.

Sikushauri, jipe muda wa kumsahau na kumuondoa akilini kwako. Usifanye maamuzi makubwa ya kimaisha na kimahusiano kwa wakati huu. Kwa mfano labda mnafanya kazi shemu moja ukaamua kuacha kazi ili kumkwepa au kuhama, ulimfumania na rafiki yako na wewe ukaamua kuwa na rafiki yake.

Hayo ni aina ya maamuzi ambayo utakuja kuyajutia huko mbeleni akili zako zikikaa sawa. Jipe muda na fanya maamuzi pale kichwa chako kitakapokua sawa, huu sio muda wa kuingia katika mahusiano mapya, kwani kwa kufanya hivyo utakua unaingia katika maumivu mapya.

Jipe muda wa kutosha kabla ya kuingia katika mahusiano mapya. Hata kama kuna mtu ambaye yuko tayari kuingia katika mahusiano na wewe, tuliza akili na usiingie tu ili akuone unafuraha, usifanye kitu kutaka kumuumiza au kutaka furaha ya mara moja, itakugharimu kaa utulie kwanza.

(5) Onyesha Hisia Zako;

Kuna kile kitu ambacho unahisi katika moyo wako, kuna hasira ambazo unazo, kuna maumivu ambayo unayo. Sio vibaya kulia kama unajisikia hivyo, sio vibaya kumuambia namna ulivyojisikia.

Kwamba huombi mrudiane lakini muambie ukweli namna ambavyo uanjisikia hasa kama yeye ndiyo amekukosea, muambie namna ulivyoumia na namna ambavyo amekuangusha. Toa yote yaliyoko moyoni yaani wakati unaondoka kwake usibaki na dukuduku lolote.

Ongea yote kabla ya kuondoka, toa hasira zote kabla ya kuondoka na uksihaondoka ukisema basi iwe basi kweli, kwamba umetoa nyongo yote mwilini na uko sawa sasa. Unaweza kulia pia na si kitu kibaya wala sio udhaifu kulia, haijalishi unalia mbele yake au ukiwa peke yako, jiruhusu kutoa hasiara zako.

(6) Ongea na Mtu;

Hii ni dawa kubwa sana, tafuta mtu unayemuamini, mtu ambaye atakufariji na kuongea naye. Mtemee kila kitu, muambie kuhusu mahusiano yenu, mazuri yake mabaya yake na kila kitu. Yaani awe kama sikio lako, tafuta mtu ambaye ana busara, mtu ambaye anaweza kukusikiliza na kukushauri.

Kua tu makini kwamba si kila mtu ni wakumuambia kila kitu, kwamba sio kwakua ni rafiki yako umamuambia kila siri yako. Kumbuka katika kipindi hiki ni rahisi kuropoka kwakua una hasira, nirahisi kutoa siri zamahusiano yako hata za ndani hivyo kuwa makini na mtu unayeongea naye.

Hakikisha ni mtu ambaye hata ukishindwa na ukampa siri zako basi atakulindia na si kuzitangaza. Kuwa makini kwani hata kama hamna matumaini ya kurudiana naye tena lakini siri nyingine hasa zako zinaweza kuathiri mahusiano yako yajayo. 

Lakini bila kujali sababu za kuachana na mwenza wako lakini alikua mwenza wako, mfichie siri zake na mhifadhi, hata yeye ana siri zako anaweza kuzitoa kama akiona umeropoka na kumdhalilisha. Hivyo kuwa makini na mtu unayeongea naye kwani bila kutarajia kwa hasira unaweza unajikuta unaongea kila kitu.

Kuongea, kuwasiliana na mtu, kusikilizwa na mtu na kufarijiwa na rafiki, ndugu na mtu wako wa karibu ni njia nzuri sana ya kuondoa mawazo. Itakuondolea upweke na mtu huyo anaweza kukuonyesha kua wewe si wakwanza na mambo yataenda vizuri tu. Unahitaji mtu wa kukuambia mambo yatanyooka usife na mzigo wa maumivu.

(7) Endelea Na Shughuli Zako Za Kawaida

Moja ya njia rahisi ya kupoteza muda na kupunguza kuwaza ni kwa kufanya kazi. Katika kipindi hiki muda unakua kama umesimama, unaweza kuwa unamuwaza kila wakati, kama unafanya kazi basi huu ndiyo wakati wa kuielekeza akili yako huko, kufanya kazi kwa bidii.

Hii itakupunguzia muda wa kumuwaza hivyo kukufanya umsahau haraka. Kuna watu ambao huona ni vyema kupumzika, kuchukua hata likizo na kwenda shemu kupumzika hasa kama shighuli zao zinawafanya kukutana na wahusika kila siku. Linaweza kuwa ni wazo zuri lakini kama huko unakoenda kuna kitu cha kuifanya akili yako kuwa bize.

(8) Tafuta Hobi, Kitu cha kukupa Furaha, kua karibu na Marafiki

Hii ni njia nyingine ya kukupunguzia kumuwaza, tafuta hobi, kitu ambacho kitatumia muda wako wa ziada. Inawezekana unayo basi ifanyie kazi na alekeza akili zako huko. Unaweza kuanza mazoezi, ukaangalia filamu na vitu kama hivyo.

Kwa kufanya hivyo akili yako itajitoa kwake. Lakini kuna marafiki, huu ndiyo wakati wa kuwatumia vizuri, sio kwa kuongea nao tena, kumjadili mhusika lakini kwa kubadilishana mawazo, kujadili mambo mengine zaidi yake. Kufungua akili yako na kujaribu mambo mapya.

Acha kuwa mpweke, kujikalia peke yako kunywa, kula au kufanya mambo ambayo yanakufanya uwe peke yako. Unapata muda wa kumuwaza zaidi unapokua peke yako kuliko ukizungukwa na marafiki. Tafuta kitu ambacho unaweza kufanya na marafiki, inaweza kuwa michezo au kutoka kiburudani.

(9) Mambo Yatakua Sawa, Utapata Mwingine

Inawezekana unawaza kuwa hutapoata mwingine kama huyo, nikweli hutapata lakini haimaanishi kuwa hutapoata bora zaidi yake. Umemzoea sana na kuna mambo ambayo unadhani huwezi kuyapata kwa mwingine, nikweli lakini unaweza kuyapata kivingine kwa mwingine.

Kila mwanadamu kaumbwa kivyake na kila mmoja ana ubora wake, kwasabbau hiyo basi usijaribu kuwalinganisha wala kuwaza kutafuta kama yule. Huwezi na kubwa kabisa jua mambo yatakuwa sawa, acha kujikasiha tamaa na jua unapoachana na mtu basi hutafuti kama yule bali bora zaidi yake.

Chukulia mapenzi kama shule, huanzi darasa la kwanza na unapofika darasa la saba ukarudi la sita hapana unaendelea mbele. Umejifunza mengi kwake mazuri na mabaya, haya utayatumia kufaulu mitihani inayokuja kwa mwingine, uzoefu utakufanya kuwa bora zaidi, hivyo usikate tama ana kujiona umepoteza muda bure.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post