NIKUTIE MOYO MPENDWA WANGU
USIKATE tamaa eti kwamba hutoolewa tena eti kwasababu kuna mpuuzi mmoja tu amekuzalisha mtoto kisha kakuacha.
USIKATE tamaa eti kwamba hutoolewa tena eti kwasababu kuna mpuuzi mmoja tu amekuzalisha mtoto kisha kakuacha.
Katika maisha yangu nimewahi kukutana na historia ya mwanamke mmoja ambae alizalishwa watoto takribani watatu wa baba tofauti,aliniambia kwamba kuna kipindi alikata tamaa ya kuolewa tena na akaamua tu aanzishe maisha ya kuwalea watoto wake.
Leo anamshukuru Mungu na anamtoto wa nne kutoka kwa mwanaume mmoja na wakweli alieamua kumchukua na kufunga nae ndoa,anasema kuna muda ni kama ndoto kwake na kuna muda anamuona mwanaume huyo ni kama malaika alietumwa na Mungu kwasababu hakutegemea kuolewa tena au kupata mwanaume ambae angeweza kukaa nae na kulea watoto ambao sio wake.
JAMBO la ajabu ambalo linamshangaza mpaka leo ni kwamba wale wanaume wote waliomlaghai na kumzalisha kisha kumuacha mpaka leo hawajaoa,umri unazidi kuwaenda na tabia yao ni kubadilisha wanawake kila wakati.
Hakika siku zote huwezi ukaharibu maisha ya mwenzio huku ukitegemea kwamba Mungu aje akupangie maisha yako mazuri baadae,kumbuka kwamba kadri unavyozidi kuharibu kwa wenzako ndivyo unavyozidi kuharibu na kwako pia.
Neno langu ni kwamba USIKATE TAMAA,kazi ya Mungu ni kuwanyanyua waliopondeka mioyo kutoka chini mavumbini mpaka juu ya vilima.HATA HILO LITAPITA TU.
UBARIKIWE SANA.```🖐🏻
UBARIKIWE SANA.```🖐🏻
Post a Comment