NENO NAKUPENDA NI RAHISI KUSIKIKA INAPOTAMKWA,TAMU MASIKIONI LAKINI ISIPOENDANA NA VITENDO HALISI HUWA CHUNGU KAMA SHUBIRI MOYONI.


Kama mtu anakupenda na anakujali lazima atafanya jitihada ya kutengeneza muda wa kuwa karibu na wewe bila ya kujali ubize au umbali uliopo baina yenu.
Atakuwa karibu na wewe kwa kila namna, atajivunia kuwa na wewe na ataonesha wazi namna anavyofurahia uwepo wako kwake.
Hivyo, kuwa makini. Usihadaiwe na hizo Nakupenda sana au nimekumiss sana. Lazima kuwepo na jitihada za kumaanisha maneno hayo.
Kumbuka, muda ni mali adhimu, usikubali kuchezewa michezo ya kitoto ukapoteza muda wako. Okoa moyo wako na muda wako kwa watu wasio serious na mahusiano yasiyokujenga zaidi ya kuzidi kukumaliza kiuchumi na kifikra.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post