Kuna siri kubwa sana kwenye ndoa ndio maana ilimpasa Yesu kuzaliwa ndani ya ndoa ingawa hakuzaliwa na mwanaume. Angeweza kuzaliwa na mwanamke ambaye ni bikira asiye hata na mchumba, lakini alizaliwa na bikra anayetarajia kuingia kwenye ndoa. Hii inamaana kwamba alihitaji kulelewa na wana ndoa.
Ndoa sio kitu cha mchezo ndiomaana biblia inasema ndoa na iheshimiwe na watu wote!
Kama kuna MTU anayeweza kufanikiwa kwa urahisi ni mwana ndoa.
Ndoa ikipona Familia nzima imepona,. Watoto wanakuwa na Amani na ustawi.
Ukitaka kujua, ukiona Watoto wanamaendeleo na ustawi mzuri embu angalia ndoa ya wazazi wao. Utaona ndoa ni ya Amani na heshima. Hapo ndipo Watoto wanapojizolea Baraka zao. Hawawezi kupata baraka ilhali hakuna Amani kuna mafarakano.
Tafuta kwa bidii Amani katika ndoa yako. Ubarkiwe
Share
Post a Comment