Wanawake wengi hufanya kila aina ishara ya upendo kwa wanaume zao, lakini cha ajabu wanaume hao bado hutoka nje ya ndoa zao na kwenda kutafuta vimada, kitu ambacho wanaweke hukosea ni kwamba wanawake hao huonesha upendo kwa wanaume zao, lakini ukweli ni kwamba asilimia tisini na tisa( 99%) ya wanaume dunia kote hawahitaji upendo kutoka kwa wapenzi wao, bali mwanaume yeyote yule anahitaji kitu hiki ili mdumu katika mahusiano ya ndoa:
1. Mwanaume huhitaji heshima kutoka kwa mpenzi wake.
Kitu kikubwa ambacho mwanaume anakihitaji kutoka kwa mpenzi wake ni heshima, na si upendo kama wengi wazaniavyo, mwanaume yeyote yule akioneshwa heshima kutoka kwa mwanamke wake huisi kupendwa zaidi. Hivi hushangai kwanini wanaume wengi hutembea na wafanyakazi wao wa ndani?
Unadhani wafanyakazi wa ndani wanajua kupenda zaidi? La hasha wafanyakazi wandani hawajui kupenda kwa asilimia mia moja ila kinachowabeba ni kule kuwa heshima, na heshima hiyo ndiyo inamfanya wanaume wengi kutoka kimapenzi na wafanyakazi hao.
Hivyo ewe mwanamke mpenda kudumu katika mahusiano ya kimapezi, ongeza heshima kwa mwanaume wako kadri uwezavyo, kwani mwanaume wako anahitaji heshima na si upendo kama we uzaniavyo.
2. Mwanaume anahitaji umuamini.
Japo jingine ambalo mwanaume wako anahitaji kutoka kwako ni vile ambavyo unamuamini, kujenga imani na mpenzi wako ndiyo siri kubwa sana ya kudumu katika mahusiano yenu.
Kutokujenga imani na mwezi wako ni mwanzo wa kubomoa mahusiano yenu, hivyo kama itakuwa ni ngumu kujenga imani hiyo unachotakiwa kufanya pale mambo yakiwa hayaendi sawa ni heri kumwambia kuliko kukaa kimya.
Hayo ni mambo ya msingi ambayo unatakiwa kufanya ili kudumisha mahisiano yenu yaweze kwenda mbele daima.
Post a Comment