Ni sifa 7 ambazo mwanamke anatakiwa kujipamba nazo ili azidi kumteka mwanaume, hasa mume anayejitambua... Ni muhimu kutambua kuwa suala la uchaguzi wa mwenza ni jambo la kwanza kabisa kwa sababu ndio dira ya maisha yako ya ndoa... Je, unapaswa kuwa vipi ili mumeo akupende?
🌺🌺🌺🌺 1. MWENYE HISIA ZA UCHESHI: Ikiwa unafurahishwa na utani wake, ni jambo litakalomvutia sana. Lakini ukiwa mwepesi wa kuchukia na kukasirika, yumkini mumeo asivutike nawe. Jitahidi kuwa na hisia za utani na ucheshi...
🌺🌺🌺 2. MWENYE KUSAMEHE: Unapoelewa kuwa mumeo sio mtu mkamilifu na unapokuwa na uwezo wa kumsamehe kwa dosari zake, hii itamaanisha kuwa unamiliki mojawapo ya sifa muhimu sana ambazo wanaume wanazitaka kwa udi na uvumba. Ukiwa na mchezo wa kumrukia kwa kila kosa dogo analolifanya au ukawa na ukosoaji uliopitiliza, tambua kuwa mumeo hatakuwa mwenye kukufurahia, hata kama ni miongoni mwa wale wasiosema. Niliwahi kumnasihi memba wangu mmoja wa Ndoa Maridhawa kuwa: “Kama wamtafuta mume asiyekosea, hutampata na utaishi bila mume”.
🌺🌺🌺 3. MWENYE SUBIRA: Sifa hii inakaribiana na sifa ya kusamehe niliyoielezea hapo juu. Ninapozungumzia subira hapa ninamaanisha uwezo wa mwanamke wa kuwa na uhusiano na mumewe bila kumshinikiza kuchukua maamuzi ambayo hajajiandaa kuyachukua. Mwanamke anaye anamuonesha mwanaume kuwa yuko tayari kusubiri humvutia zaidi mwanaume kuliko yule anayetoa picha inayoonesha kuwa si mwenye subira.
🌺🌺🌺 4. MWENYE ASHIKI: Mwanamke ambaye sio romantic huwa hamvutii mwanaume. Ili mwanaume avutike unatakiwa kumfanya ahisi raha na uwe mwepesi wa kumchokoza. Ikiwa unadhani kuwa mwanaume ndiye tu anayepeswa kukuchokoza, basi hapo unajitesa na haitakuwa na faida kwako. Boresha uwezo wako wa uchokozi na kuwa romantic utaona namna mumeo atakavyokuwa akikutamani.
🌺🌺🌺 5. MKWELI: Wanaume wanavutiwa sana na mwanamke mkweli, mwaminifu. Ikiwa wewe ni mwanamke unayosema ukweli, usiyeficha ukweli, basi sifa hii itamfanya mwanaume avutike nawe. Ifanye kauli mbiu ya maisha yako iwe ni: “Sema unachofanya, na ufanye unachosema”. Kama ambavyo mwanamke anampenda sana mwanaume mkweli, vivyo hivyo mwanaume anavutiwa na mwanamke mkweli na mnyenyekevu ambayo hapendi makuu.
🌺🌺🌺🌺 6. ALIYEFUNGUKA KIAKILI: Raghba ya ugunduzi wa fikra na mawazo mapya ni sifa nyingine ambayo mwanaume anapenda kuiona kwa mwanamke anayetaka kuangukia katika penzi lake. Ninachokusudia hapa ni ule uwezo wa kuona mbali, kutambua na kuheshimu mtazamo mwingine, hata kama utakuwa kinyume na mtazamo wake. Aidha, miongoni mwa mambo ambayo wanandoa wengi wanakosa ni dira (vision). Hakika iwapo mwanamke ana sifa ya kuwa na dira atamvutia sana mwanaume.
🌺🌺🌺 7. UELEWA WA KIAFYA: Mwanamke ambaye anajitunza humvutia sana mwanaume kuliko mwanamke asiyejitunza. Muonekano wa kimwili humvutia mwanaume. Mume huvutiwa na mwanamke anayefanya mazoezi, anayekula chakula chenye afya, anayezitunza nywele zake na mwili wake kwa ujumla, na anayevaa mavazi maridhawa. Jitahidi sana kumvutia mumeo kwa kuonekana mpya kila siku. mtoto wa kishirazi mwenye kujiamini na kujitambua
Nmeipenda sana Asante kutupatia elimu
ReplyDeletePost a Comment