Kuna rangi za ute ambazo hutoka kwenye u-ke, zipo za kawaida na zisizo za kawaida, kutofahamu ute wa kawaida huongeza hofu kwa wengi lakini ukifahamu ute wa kawaida ni msaada kujua ute upi si wa kawaida na kugundua mapema kwamba upo kwenye tatizo linalohitaji tiba.
🌹 Rangi ya ute unaotoka kwenye uk-e unapaswa kuwa mweupe na wenye kuonekana vyema (clear), ute huo ni sehemu ya mwili kufanya kazi vizuri, unatoka kwaajili ya kusafisha na kuweka u=ke salama.
🌹 Uzito na muonekano wake unategemea zaidi uko katika kipindi gani ndani ya uanguaji mayai au kipindi cha damu ya hedhi kwa ujumla.
🌹 Mabadiliko yoyote ya rangi ya ute zikiambatana na dalili tofauti inaweza kuwa ni sehemu ya maambukizi fulani,yanayohitaji uangalizi na umakini ni vyema kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.
🌹 Unapaswa kuangalia zaidi rangi ya ute na harufu yake, ni rahisi kujua tatizo ndani yake, ute wa kawaida hautoi harufu wala haukeri, lakini wenye maambukizi fulani unatoa harufu. UTE MWEUPE.(white)⚪ Huu ni ute wa kawaida kutoka kwa mwanamke hasa katika kipindi cha hedhi lakini utakapokuwa mzito kiasi na wenye kufanana na mtindi,ukiambatana na maumivu ni dalili ya maambukizi (yeast infection) Matibabu baada ya uchunguzi yanahitajika.
🌹 UTE WA MAJIMAJI.(clear waterly) Ute wa majimaji ni ute unaohitajika zaidi kwa mwanamke, ute unaofanya uk-e usiwe mkamvu, ute huu mwanamke anapaswa kuhakikisha anakuwa nao hasa kwenye tendo la ndoa, unasaidia kulinda manii na kuzisafirisha, unaleta uwezekano mkubwa wa mimba kutunga.Ute unaoshiria kwamba upo kwenye kipindi cha kuangua mayai, ukiwa nao wala hauna shida wala tatizo.
🌹 UTE WA NJANO.( yellow or greenish) 💛 Ute huu si salama unapomtoka mwanamke, ni ute unaoshiria maambukizi ya bakteria pamoja na magonjwa ya zinaa, hutoa harufu isiyopendeza unaweza ukaambatana na ukijani ndani yake, pindi unapouona nenda hospitali na mwenza wako, magonjwa ya zinaa hutibiwa na wapenzi wote wawili ili kuepusha muendelezo wa maambukizi endapo atatibiwa mmoja.
🌹 UTE WA KAHAWIA. (brown) Ute huu humtoka mwanamke pindi anapomaliza hedhi yake, husafisha uk-e baada ya hedhi, unaweza kuambatana na damu damu kiasi lakini unaweza kutokwa na ute huu katikati ya hedhi yako au kipindi cha mwanzo cha ujauzito.
🌹 Wenye mzunguko wa hedhi unaobadilika badilika huweza kusababisha kutokwa na ute huu, pindi unapotokwa zaidi na ute huu inaweza kuwa ni dalili ya kansa ya shingo ya kizazi. ni vyema kufika hospitali kwa uchunguzi zaidi.
🌹 Sababu za kutokwa na uchafu uk-eni tumeshajifunza kwenye somo lake, ni vyema kusoma yote kwa makini ili uweze kujua zaidi kwanini unatokwa na ute au uchafu uk-eni na nini ufanye. Asante🌹 BEAUTY ZONE 2
Post a Comment