Ukiolewa jua kuwa unaingia kwenye familia ya watu, ni familia mpya na kuna watu wamelelewa tofauti kabisa, kuna mambo ambayo wewe utayaona kama ni mambo ya ajabu lakini kwao ni kawaida. Kwa mfano, utakuta familia wanaombana kila kitu, wanavaliana mpaka nguo, utakuta familia ndugu wanajazana sehemu mmja Kaka yao akioa basi wote wanaenda kwake na kukaa kana kwamba ni kwao, unaweza kukasirika, lakini kumbuka kuwa kama wanafanya hivyo na wanaona kama ni kawaida kuna uwezekano mkubwa na mume wako yuko hivyo.
Kabla ya kuingia na mdomo wako, kuleta uzungu wenu kwenye famila za watu, hembu kwanza tulia, anza kujifunza mazingira, kuwa mjinga hata kwa miezi sita ujifunze na ujue familia ile inaendeshwaje. Kuna familia ambazo Baba mkwe anazunguka na taulo wakati kwenu si kawaida, kuna familia ambazo Mama mkwe anaingia chumbani na hata kumchagulia mwanae nguo ya kuvaa, kuna familia ndugu wanakuja kupika kama kwao, jifunze kwanza, kabla ya kuanza kulalamika na kukunja sura huku ukivimbisha mashavu kuwa sitaki hiki sitaki hiki basi tuliza kalio chini na jifunze.
Ungetaka kuolewa na familia ya kistaarabu ungeolewa na Kaka yako, huyo ndiyo malezi yenu yamefanana usingepata shida. Lakini unefika kwa watu unaanza kubadilisha kila kitu, mara sitaki wadogo zako waje, mara sitaki hii, sitaki kile, sitaki sijui nini! Ukweli nikuwa, hata kama wewe uko sahihi, hataka kama mtu mwingine angekubaliana na wewe, lakini unachokiona, tabia zao ndiyo malezi yao na ndiyo kawaida kwao, usiwe na kasi ya kuleta ustaarabu wa kwenu kwao, kumbuka wewe ndiyo umeolewa, uko peke yako huwezi kuwabadilisha, ustaarabu wako subiri uzae uwaletee watoto wako na si wakwe zako!
Tuongee tu ukweli, hivi unafika unakutana na Mama mkwe ni mbea anasengenya kila mtu Mama ana uzoefu wa umbea, uzoefu wa uchoyo, uzoefu wa kufuatilia mambo ya watu wa miaka 60 halafu umbadilishe kwa miezi sita wewe ni nani hasa! Mume wako yeye mwenyewe Kaka yake alipooa au ndugu yake mwingine alipooa alikua anaingia mpaka chumbani kwa shemeji yake wala hajali wewe unakuja unaleta utaratibu mpya kuwa chumba chako mtu asiingie! Watu wanakula kwenye bakuli moja, hata kama ni uchafu wewe ndoa hata mwezi haina unataka kuwabadilisha sijui self services! Kwa sahani zipi!
IDD MAKENGO
Post a Comment