MWANAMKE SOMA ILI UPATE KUJUA NAMNA NZURI YA KUISHI NA MWANAMKE

Nisome Mwanamke ili upate kujua namna nzuri ya kuishi na Mwanaume;
• MFANYE MWANAUME AKUZOEE KIASI KWAMBA ASIWEZE KUHAMISHA HISIA ZAKE KWA MWANAMKE MWINGINE💯
Mapenzi PEKEE hayamfanyi Mwanaume kutulia hasa ukizingatia WANAUME kwa uhalisia wao wanapenda MAPENZI MAPYA bila kuangalia UBORA WA MWANAMKE HUSIKA😂
Mfanye Mwanaume akumbuke huduma zako muhimu kwake kuliko kuwekeza kwenye style na mikao ya kitandani maana hayo sio MAGENI kiumeni😂
Wengi mnajidanganya kwa sababu mmechezwaUNYAGO etiii Mwanaume atakuwa na wewe kwa sababu ya MAUNO yako wallah sio kila Mwanaume anapenda MAUNO na niwajuavyo wanaume makini wanamtazama Mwanamke kama MSHIRIKA WA MAISHA tofauti na wanaume wachache wanaomtazama Mwanamke kama DARAJA LA MAHITAJI YAO.
Mwanaume ukimfanya akuzoee atakuwa na mambo matatu ya faida kwako;
• WOGA WA KUMSHITUKIA.
• WOGA WA KUKUKOSA.
• WOGA WA KUHARIBU NURU ALIYO NAYO KWA UWEPO WAKO.
Mwanaume kwa HULKA ni mhuni ila wakati huo huo Mwanaume ni MWOGA WA KUHARIBU ikiwa tayari NAFSI YAKE IMETWAMA KWAKO💯
Mwanaume hatulizwi kwa MAPENZI 
Bali unaweza kumtuliza Mwanaume kwa sababu ndogo mno "UPOLE WAKO" halafu watu watasema wewe mchawi😂😂
Wanawake achaneni na mambo ya KUFIKIRIKA na mjitume kumjua Mwanaume mmoja mmoja maana HAWAFANANI japo hulka yao ni sawa ndo maana unaweza kumtofautisha JUMA NA PETER😎
Jenga ushawishi wa kumfanya Mwanaume ahisi upweke uwapo mbali nae hiyo itamfanya kukosa uthubutu wa kukusaliti, Ujinga wa Mwanamke ni kuwazia KUMKAMATA MWANAUME KI MAHABA huku akisahau Mwanaume anaweza kufanya ngono na mbuzi na akifika keleleni ije kuwa wewe💃
Mtu anayeweza kulala na wewe na akalala na nduhuyo halafu bado unajifunza utundu kitandani ili umkamate? Shwainiiiii🙄
Maana ya maandiko kusema;
• MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA YAKE MWENYEWE ni wazi Mwanamke usiipe kipaumbele NGONO bali jitunze kumkabili Mwanaume mmoja umpendaye wekeza UTII na kumpa heshima kama MUME wallah hutakuwa na mshindani MOYONI mwa Mumeo💯
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🔨


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post