*🔴MWANAMKE ANACHOTAKIWA KUFANYA MUME ASITOKE NJE YA NDOA.🔴* _

Doctor-Love - #AFYA: FAHAMU DALILI KUU ZA AWALI ZA MIMBA ...

✍🏾Mapenzi yana kanuni zake, *kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia.* Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza *lakini omba sana* upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.

_ _✍🏾Kwa bahati mbaya ukitokea *kumzimikia mtu* ambaye wala hana hata *chembe za penzi kwako,* utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia *vidonda vya tumbo*.


_ _✍🏾Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata *wapenzi wa ukweli* lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha *penzi*, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.

_ _✍🏾Kwa kifupi ni kwamba, *unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda*, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia *utundu na ubunifu* wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake._ 

,_✍🏾Ninapozungumzia hayo, *namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi* ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.

_ _✍🏾Faragha ni eneo *muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa.* Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.

_ _✍🏾Mwanaume anatakiwa *kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili.* Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo *kiduchu kwani* ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.

_ _✍🏾Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.

_ _✍🏾Hawa wanatakiwa kujiona ni *wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa,* wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.

_ _✍🏾Kinachonishangaza ni kwamba, *kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.

*_ _✍🏾Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu *wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao.* Hawajui kitu, *wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu*, zitadumu kwa misingi ipi?

_ _✍🏾Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama *mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje.* Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni *mke wa pambo la nyumba tu.*

_ _✍🏾Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.

_ _✍🏾Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo *zinazooonekana kuwashika waume za watu* siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.

_ _✍🏾Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo?_ *Namalizia kwa maneno haya*

 _✍🏾Naomba niseme tu kwamba, *huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba,* ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.

_ _Hakikisha *unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia*._ _ahsanteni sana kwa muda wenu_ _©brayton official love * 🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post