Kuna wakati huwa unafika kwa kila mmoja wetu akili inachoka juu ya kuendelea kutaka jambo ulilokuwa unatamani kuwa nalo. Huu ni wakati ambao hata moyo wako unakata tamaa kwa kila jambo unalotaka katika maisha yako.
Huu ni wakati ambao hasira, uoga, kukata tamaa haraka ukujaa ndani yako.. uchukua nafasi kubwa kuliko ujasiri uliokuwa nao hapo awali... Ubora wa kufikiri upungua.
Kama ulikuwa haujaolewa unakata tamaa ya kuolewa ...kama ulikuwa unatafuta kazi unakata tamaa ya kupata kazi tena, kama ulikuwa unategemea kufungua biashara unakata tamaa ya kufungua biashara maana hasara inazidi kila kukicha
Huu ndio wakati ambao akili iliyokata tamaa na moyo wa kupaniki kwa pamoja ufanya kazi tena kwa nguvu kuliko zamani.
Huu ndio wakati ambao neno HAIWEZEKANI lina nguvu kubwa sana kuliko neno INAWEZEKANA.
Jambo kubwa nalolijua katika nyakati kama hizi endapo zikikufika .. AMINI KATIKA MAOMBI .. Kuna matumaini tena katika maombi... Maombi yana nguvu kubwa sana .
Piga magoti chumbani kwako kwa sauti ya chini mwambie Mungu ... "Tengeneza tena ndani yangu maana viungo vya mwili wangu havina usaidizi tena katika future yangu...naogopa linalokuja mbele yangu maana nimekata tamaa".. weka nguvu mpya ndani yangu ..ponya akili yangu maana imechoka".. walioamua kufanya kazi nawewe hawakuwahi kuwa peke yao ..naomba usaidizi wako kwa kunitengeneza upya ndani yangu"
Ukimaliza kufanya maombi yako jambo la kwanza unalotakiwa kuliamini kwa asilimia 💯% ni kuwa Mungu amekusikia ... Maana matatizo ya maisha yako hayako nje kama wewe unavyoamini ...yako ndani yako.. yamo katika akili yako, yamo katika moyo wako, ...fix hayo kwanza kwa kutengeneza na Mungu wako..niamini ukifanya hivi kuna utendaji mpya utajijenga ndani yako ..kuna nguvu kubwa itakuja tena ndani yako.. utakuwa mpya tena maana hautakuwa peke yako tena...nyakati hii utakuwa na Mungu.
Dayari Yangu
Post a Comment