MANENO YANAYOMFURAHISHA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO



Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza.
Sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unaempenda na unahitaji awe wako milele.
1. Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama.
2. Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili mapenzi yako.
3. Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu.
4. Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua.
5. Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha.
6. Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini umenichagua mimi.
7. Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo.
8. Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti.
9. Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu.
10. Siamini, maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi.
11. Kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife.
12. Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja.
13. Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia.
14. Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.
15. Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa.
16. Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi.
17. Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda.
18. Napata furaha nikiwa na wewe.
19. Napenda kutumia muda na wewe.
20. Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa.
21. Natamani maisha yangu yote nikuone ukiwa na furaha.
22. Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo.
23. Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto.
24. Napenda nywele zako.
25. Napenda nikukumbatie ninapokuaga.
26. Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako.
27. Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza siku na wewe kwenye ndoto zangu.
28. Ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka.
29.Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima ni mtu wa furaha.
30.Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post