-Mwanaume anaweza kumkataa mtoto wake halali kabisa kisha akasingiziwa mtoto wa mwanaume mwingine na akakubali...!!!
-Mwanaume ni kiumbe cha pekee ambaye anatafuta hela kwa jasho na nguvu kwa ajili ya hawara huku mkewe na watoto wakiteseka ...!!!
- Mwanaume ni kiumbe cha pekee ambaye anaweza kujiua kisa tu amesalitiwa na mwanamke, sijui uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wamepotezea wapi..!!
- Mwanaume anaweza kupanga mipango ya kuchepuka kichwani, ambayo inaweza kudumu kichwani mwake hata miaka kumi kuliko mipango ya maendeleo ...!!
- Mwanaume yupo radhi hata kulala na njaa, ili mladi tu atimize adhima yake ya kumhonga na kumnasa binti mwenye wowowo kubwa ...!
-Mwanaume kweli ni wa ajabu sana, anaweza kufuta kwenye kiti anachotaka kukaa, ilihali boxer aliyovaa hajaifua wiki 2..!!
- Mwanaume anaweza akawa na wanawake hata 3, lakini mkewe wa ndoa asijue hata siku moja..!!
- Mwanaume anaweza kuishi na mke wa ndoa zaidi ya miaka kumi Wakiwa wamepanga, lakini ana hawara amemjengea nyumba safi kabisa..!!
- Mwanaume anaweza kuwa na heshima nchi nzima, mkoa mzima, Mtaani kote, lakini nyumbani kwa mkewe, anaonekana boya kabisa, na deki anapigishwa, na vyombo anaosha..!!
- Mwanaume anaweza chuma mali na mkewe, na mwisho akamwacha mkewe , Na kuoa baamedi...!!
- Mwanaume anaweza akawa na kazi nzuri lakini akawa anaishi kwa mwanamke akamjengea, akamfungulia biashara, ila akifukuzwa tu kazi anakosa pa kuishi na mwanamke nae anamfukuza....!!!
- Kama hujui mwanaume akili yake inawaza mapenzi kwa asimilia kubwa kuliko mwanamke...!!!
-Kama hujui pia wanaume wengi wanateseka kwenye mahusiano lakini wanajifariji kwenye pombe...!!
*NDIYO MAANA WANAKUFA MAPEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!*😁😁😁
Post a Comment