Watu wengi, wanaume kwa wanawake wakiachwa na watu wanaowapenda kitu cha kwanza kufanya ni kuangalia kasoro zao. Kujiangalia wamekosea wapi na wanamapungufu gani ambayo yamewapelekea kuachwa.
Hali hii huwafanya kutokujiamini na kujiona kama wana kasoro flani hivyo kuwawia vigumu wanapoingia katika mahusiano mapya. Lakini hembu nikuulize kama ulishakutana na hali hii je ulishakaa kitambo kidogo na kujiuliza labda tatizo sio wewe.
Kwamba kweli kakuacha lakini inawezekana kakuacha kwakua hakuwezi na sio kwamba hufai. Kwamba ingawa wewe unamuona wamaana, unamuona anajiamini lakini yeye hajiamini kuwa na mtu kama wewe.
Anajidharau na anaona kama akiendelea kuwa na wewe ipo siku utamuacha na ataumia sana. Sasa nikuambie kitu Kama mpenzi wako kakuacha Kwa matusi, kejeli na vitu kama hivyo.
Kuna uwezekano mkubwa hajiamini au alishaona dalili kuwa unaelekea kumaucha na kaona akuche mapema ili aibu iwe kwako. Kwamba usije ukaringa kuwa umemuacha kwakua yeye ndiyo kakuacha!
Unapoachwa hasa wale ambao mnaachwa bila sababu yoyote, taratibu mtu anakuambia kua hakutaki, hujamfumania, hajakufumania na hakuna mabaya yoyote mliofanyiana.
Lakini kuna wale ambao wanakuacha kwa dharau, utasikia kuwa wewe si wahadhi yangu, siwezi kuishi na mwanaume wa namna hii, au wewe mwanamke una matatizo, kabla ya kuangalia kasoro zako hembu angalia inawezekana labda ni yeye kaona kuwa ana tatizo na hakuwezi.
Acha kujiwazia mabaya kwanza, inawezekana kweli unamapungufu lakini wewe si malaika, kama hawezi kuishi na mapungufu yako basi si wa hadhi yako. Lakini inawezekana hata hayo mapungufu si sababu, sababu kubwa ni yeye kutokujiamini.
Inawezekana aliyekuacha anakuona kuwa wewe si wa hadhi yake kweli, lakini haimaanishi kuwa wewe ni wa hadhi ya chini hapana inamaanisha kuwa wewe ni wa hadhi ya juu na hakuwezi. Jitambue na acha kulialia kwani wewe ni bora
Post a Comment