1. Mawasiliano na Uaminifu ni nguzo kubwa katika mahusiano au ndoa yoyote ile.
2. Mahusiano yanaumiza mno hasa kama unaempenda haonyeshi jitihada zozote za kutunza na ku-appreciate upendo anaopewa. Ila Wakati unapofika, moyo wa mtu huchoka na utakapochoka hautarudi nyuma tena!
3. Kama hauna nia ya kumvisha PETE, basi uwe na ujasiri wa kumuacha ili aweze kukutana na MTU wake sahihi ambaye Atamvisha Pete na kumuoa. Ni vibaya mno kumpotezea muda wake na nafasi yake ya kukutana na MR. RIGHT.
4. Wengi walikosea kuoa/kuolewa na watu ambao tabia zao zilikuwa sio za kuridhisha kipindi cha mahusiano na wakaamini kwamba watabadilika. Hivyo, tambua tabia halisi anayokuonyesha mtu kipindi cha mahusiano, ndiyo itakayokuwa wakati wa ndoa!
5. Usioe Mwanamke ambaye anawekeza fedha katika nywele zake au mwili wake kuliko kwenye ubongo wake. Mafanikio sio ajali, ni matokeo ya vipaumbele, ama focus na uwekezaji.
Mwanamke ambaye anahangaisha kubadili nywele zake na muonekano wake wa nje pasina kuhangaisha ubongo wake, ni mzigo katika familia!
6. Pamoja na mengine, mwanamke ambaye yupo tayari kutumia lips zake kukuombea kuliko kuzichezesha chezesha kwenye snap chat, ni mwakamke ambaye anafaa kuwa MKE wako!
7. Wanaume walio wengi wanapenda kulala na wanawake, lakini ni wanaume wachache ambao wanapenda kuamka na kusimama pamoja na wanawake zao kuwasukuma kiuchumi.
Hivyo, pamoja na mengine, utajua kama ni MTU sahihi kwako kama yupo Interested na kukuinua juu kiuchumi kuliko kukulaza chini kwa ajili ya tendo la ndoa pekee!
8. Siku zote, Mwanaume ujitaihidi kutafuta fedha. Na kipato chako kizidi cha mwanamke wako. --- wanaweza kusisitiza juu ya usawa wa kijinsia, lakini mioyoni mwao wanataka Mwanaume mwenye uwezo wa kuwalipia bili!
9. Mwanaume mwenye mvuto na fedha anaweza kuvutia wanawake wengi, ila mwanaume mwenye hekima anajua ni yupi wa kumchagua. Mwanaume mwenye busara anafahamu kuwa sio kila mwanamke anahitaji nafasi katika maisha yake. Hivyo mwanamke omba sana Mungu akupe mwanaume mwenye hekima.
10. Haijalishi unapitia magumu gani, amini kwamba ipo siku ukurasa huo uyafungwa na kufunguliwa ukurasa wa furaha, faraja na amani ya maisha. Kesho ni yako!
I wish you a glorious year 2020!!!!
Post a Comment