📂Kwenye mahusiano, Ukitambua kuwa kuna kukosea na kukoseana. Basi neno msamaha na samahani lazima liwe silaha ya upendo wenu.
📂Kwenye mahusiano ukitambua hakuna mkamilifu kati yenu basi Huruma na Kuhurumiana iwe nguzo ya upendo wenu.
📂Kwenye mahusiano ukitambua kuna kupewa na kupeana basi neno Asante liwe shina la upendo wenu.
📂Kwenye mahusiano ukitambua kwamba kuna kupata na kukosa basi subira itumike kulinda upendo wenu.
📂Kwenye mahusiano ukitambua kuna kuanguka na kusimama basi busara iwe mhimili wa upendo wenu
Post a Comment