KWANZA KABISA UJUE UNAMPENDA NANI KABLA YA HASIRA ZAKO KUKUPANDA!

Happy together - young couple kissing. Lifestyle photo of young ...
Ni kweli kabisa nakuelewa na ku-imagine that pain you have ila nikwambie kabisa KAMA ASINGEKUWA WA HISIA ZAKO wala usingeumia, POLE... Weka pin📌 kwa umpendaye, sio kila mtu anaweza kufurahia na mwenendo wa penzi lenu hata kama unadhani haendani na kasi yako but YEYE NDO WA MOYO WAKO! Shetani alivyo atakupandikizia kiburi usahau yale mazuri yake na utahesabu mabaya yake tu na mwisho wake utahukumu vibaya bila hata kuweka uwiano wa MEMA NA MABAYA YAKE... Najua shauku yako ni KUONA NDOTO YAKO IKITIMIA ni ndoto ya mtoto? Ni ndoto ya utulivu wake? Na mengine mengi unayo ota juu ya penzi lenu, Nikukumbushe KATAA KUJIFUNZA KWA WALIO SHINDWA NA HAWAJUI KAMA WAMESHINDWA! Maana hao ndo hujifanya wajuaji hatari, Wakati wewe ukiugulia kwa mawazo ya kuachana na wa moyo wako niamini wao watakuwa wanakucheka kwa kuachwa, wala hawatakumbuka kama walikushauri umuache, Ziko MOMENTS mnazijua wawili, Yako mambo mazito na magumu mlishirikiana bila wapambe lakini wao wanalolijua ni moja tu MTU HUYO HAKUFAI! Nani alikwambia JAMBO ZURI LINAKUJA KWA MUUJIZA? Unatakiwa upambane, NO GAIN WITHOUT PAIN💪🏽
Wao wanamuona mbaya na mtu asiyefaa kwako Unadhani waliwahi jiuliza Kwanini UNAMPENDA? My friend MOYO UKIISHASEMA NDIYO hakuna wa kubishana nao, Usikubari kufundishwa namna ya kuishi na mwenza wako bali pokea ushauri wa jinsi ambavyo UKIVUMILIA UNASHINDA... Pigania PENZI lako kwa nguvu na akili zako zote ili nafsi yako ipate kutulia, Sio kila MAHUSIANO yanaweza kukupa Furaha na Amani, lakini yuko mmoja ambaye anayo MAMLAKA hayo ya kukupa FURAHA NA AMANI na huyo ndiye wa kushikamana nae, Ukikubari akuondoke kwa upuuzi wako TARAJIA kulikosa PENZI LA MOYO WAKO na huweZi kulijenga tena kwa muonekano ule wa mwanzo, Maana MAPENZI HAYANA MAPUMZIKO Kwani kila kukicha ni MAPAMBANO ili tushinde vikwazo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post