KWANINI NDOA INADUMU KWA UVUMILIVU WA MWANAMKE?

JE WINGI WA MISAMAHA NI SURUHISHO LA MAKOSA AMBAYO YANAUMIZA ...
Kwanza kabisa niwapongeze wanawake wote ambao MUNGU aliwataja kuwa wenye HEKIMA... Huko uliko Mama yangu MUNGU AKUPE PUMZIKO LA AMANI YA MILELE🙏
Mwanamke asipokuwa mvumilivu NDOA HAIWEZI KUTAJWA! Mwanamke asipokuwa mvumilivu HAWEZI KUZAA MTOTO WA PILI Kwani ndoa nyingi huwa tamu wakati wa mwanzo na ukikuta Mwanamke hajabeba MIMBA na akabaini aliingia choo cha kiume WALLAH HAWEZI KUBEBA TENA MIMBA... Kama kuna kitu wanawake wanakiogopa ni KUZAA MTOTO AMBAYE HATAKUWA NA MAPENZI YA BABA YAKE😭
Ziko ndoa nyingi sana pengine napata ujasili kuitaja asilimia 85 wanawake wanaishi kuitunza heshima yake, kulinda watoto wake, kuogopa kuanza mikiki mipya ya mapenzi, Na wengine fikra zao kutawaliwa na wazo kwamba wao tena sio wanawake wanaoendana na kipindi kilichopo Yaani kwa lugha fupi ANAJIONA AMEPITWA NA WAKATI🙆🏿‍♂
Ni kweli kabisa MWANAMKE NDIYE MLINZI NA MTETEZI WA MAHUSIANO/NDOA Kwani Mwanamke akivunjika moyo wa kuendelea mara nyingi PENZI HUFA... Ziko ndoa nyingi Mama na Baba wanatoka geti moja but huko ndani hawali meza moja wala kulala chumba kimoja achilia mbali kitanda kimoja wala wasikumbuke ni lini ilikuwa mwisho kukumbatiana🙈
Hatuwezi kushindwa kuwakosoa wanawake lakini tujue jambo moja ili wakati tunamkosoa Mwanamke tumpe haki yake, Mwanamke akipewa nafasi ya kuelezea kinachomuumiza mara nyingi hujisikia AMANI hata kama majibu ya upande wa pili yatakuwa YA KUMPUMBAZA ILI SIKU ZIENDE🤣
Kwa maana hiyo unagunduwa kwamba kosa liko kwa MWANAUME KUSHINDWA KUTOA NAFASI YA KUMSIKILIZA MKEWE na ukifuatilia utabaini kwamba WANAUME TUNAPEANA UJINGA WA JINSI YA KUISHI NA WAKE ZETU🚫
Mwenzio ameoa KAHABA na Wewe umemtoa Mke wako kwenye Maadili UTAWEZAJE KU-COPY TREATMENT KWA TOFAUTI HIYO? Ukijua KUTONGOZA basi rafiki yangu ujue na KUBEMBELEZA💃
Wanawake ni watu wazuri sana ukiweza kucheza na akili yake, imagine unakutana nae barabarani unamtongoza na anaanguka kwenye himaya yako UNASHINDWAJE KUMFANYA AWE WAKO MILELE BILA KUMKOSESHA FURAHA? Nadhani na ninyi wanawake hebu wachunguzeni hao wanaume mnakutana nao, Maana bora akuombe uroda😋 tu na asikutajie NAKUPENDA! Maana najua mnako kaugonjwa ka KUPUMBAZIKA KWA MANENO MATAMU 😂 sasa rafiki sio kila neno tamu lina sukari, Wapo wanayatoa maneno matamu juu juu ila chini ya uhalisia ni kuchungu hatari📌
Nadhani tubadili mfumo wa MAPENZI tutoke kwenye NAKUPENDA na twende kwenye NAKUTAKA🤦🏾‍♂
Maana neno NAKUPENDA kwa sasa linatumika kama JOJO kwamba ukianza kuitafuna ni tamu but unajua mwisho wake utakuwa UMEFYONZA SUKARI YOTE mwisho wake ni kufanyaje? Sema KUTEMAAA🙋🏻‍♂
Wanawake niwape mbinu🤷🏽‍♂
Kabla ya kumpenda mtu nawe mkubali kwa sekta ya kutimiza haja ya mwili🙈
Ukiona anakupenda nawe sasa chenjia gia angani🛫 ili mwende Sawa, Mambo ya kutamkiwa NAKUPENDA unaingia kichwa, miguu, mwili, akili na MOYO bila kujua hitaji la mwenzio AKIKUBADILIKIA VIDONDA VYA TUMBO VINAKUHUSU🏃‍♀🏃🏻‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post