Kwanza kabisa naomba nieleweke kwamba "MAHUSIANO YANAENDANA NA JINSI MLIVYOWEZA KUKUTANA" Sina maana wanaokutana misikitini 🕌 ama makanisani ⛪haina maana wao wapo kwenye usalama wa mahusiano yao, Swala UPENDO ni mtambuka wa mambo mawili;
■ KUWIWA
■ KUHITAJI
Na ukiwiwa kumpenda mtu maana yake unajikuta umekuwa mdhaifu kwake, Na ukijikuta unamhitaji mtu kwa kawaida upendo huinuka, Yote hayo yanahitaji KUTHAMINI!
Pindi watu wawili wakianzisha mahusiano mapya ni furaha na hakuna msongo wa mawazo maana muda mwingi huzijenga nyakati za kuhitajiana, Miezi kadhaa ya manzo kwenye mahusiano siku zote inakuwa rahisi saana kumuona mwenzio ni wa maana kwa sababu hujamlinganisha wala kumzoea, Ghafla wivu unaingia wivu huingia kwa sababu ya hofu ambayo mara nyingi hujengwa na mtu ambaye hutumia akili nyingi kuishi na mwenza wake kuliko kuweka uwiano wa namna gani wanatakiwa kuenenda na mahusiano yao, mabadiriko yatajionyesha mara kwa mara kwa sababu moja tu TUMAINI LA MHITAJI LIKIINGIWA DOSARI... Mabishano yatatokea kusikojulikana na mambo ya kuaminiana yatatoweka kwa sababu moja tu MATUAMINI YAKIISHA... Mambo yanakuwa halisia kuendana na uwazi pamoja na ukweli na hapo ndipo utakapoona kama atabaki au hatobaki na kulifanya lisidumu! Watu wengi wataondoka lakini kama una mtu ambae atabaki licha ya misongo na mikwaruzano, ni mtunzaji wa ahadi zake kwako ila ukweli ni kwamba MAPENZI YANAUMA kuliko maumivu yoyote ambayo mtu anaweza kuyapitia, Jino likizidi kuuma dawa yake KULING'OA😂 Hebu niambie unapokuwa UNAMPENDA MTU NA UNABAINI ANAKUHADAAA MAUMIVU YAKE UNAYAFANYAJE? Hakuna tiba ya majeraha ama vidonda vya Mapenzi ila MTU UMPENDAYE KUKUPA UPONYAJI baada ya kujua kwamba unateseka juu yake, Lakini kama akilibebea udhaifu jambo hilo kwamba afurahie mateso yako wallah WAFAAAAA😭
Usikubari Mtu akacheza na MOYO wako! MOYO wako unapougua juu ya mtu na haonyeshi kuhisi maumivu yako HUYO MPE NAFASI YA URAFIKI WA KALAMU vinginevyo utakufa siku si zako🙋🏻♂
Post a Comment